Baadhi
ya wachezaji wa timu ya Kamba ya Ofisi ya Makamu wa Rais, wakishangilia
ushindi wao baada ya kuwaburuza timu ya Katiba na Sheria katika raundi
mbili mfululizo, katika mchezo wao uliochezwa leo asubuhi kwenye viwanja
vya Chuo Kikuu cha UDOM mjini Dodoma. Picha Zote na OMR
Wachezaji
wa timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Kamba wakionyesha uwezo wao wa
kutunisha misuri kuwaburuza wapinzani wao wa timu ya Katiba na Sheria,
wakati wa mchezo wao uliochezwa leo asubuhi kwenye viwanja vya Chuo
Kikuu cha UDOM mjini Dodoma. Katika mchezo huo Ofisi ya Makamu wa Rais
ilishinda kwa raundi mbili mfululizo.
Wachezaji
wa timu ya Katiba na Sheria, Kamba wakijaribu kugangamala kuwazuia
wapinzani wao wa timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais, wakati wa mchezo wao
uliochezwa leo asubuhi kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha UDOM mjini
Dodoma. Katika mchezo huo Ofisi ya Makamu wa Rais ilishinda kwa raundi
mbili mfululizo.
Wachezaji
wa timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais (kulia), Kamba wakionyeshana umwamba
wapinzani wao wa timu ya Katiba na Sheria, wakati wa mchezo wao
uliochezwa leo asubuhi kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha UDOM mjini
Dodoma. Katika mchezo huo Ofisi ya Makamu wa Rais ilishinda kwa raundi
mbili mfululizo.
Wachezaji
wa timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais Kamba wanawake, wakishangilia
ushindi wa chee waliopata baada ya wapinzani wao Katiba na Sheria
kuingia mitini.
Wachezaji
wa timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Kamba na Soka, wakiwa katika picha
ya pamoja, baada ya timu zao za Kamba (KE) na (ME) kushinda katika
michezo yao.
Kamba
wananwake Bunge na Uchukuzi, wakiburuzana. Katika mechi hii, Bunge
walishinda baada ya kuwaburuza wenzao mara mbili mfululizo.
'RAHA
YA USHINDI BAO', Wachezaji wa timu ya Kamba ya Habari, wanaume
wakishangilia ushindi wao baada ya kuwaburuza mara mbili mfululizo
wapinzani wao, Uhamiaji katika mchezo wao uliochezwa leo asubuhi, kwenye
viwanja vya Chuo Kikuu UDOM, mjini Dodoma.
Wachezaji
wa timu ya Habari (kushoto), Kamba wakionyeshana umwamba wapinzani wao
wa timu ya Uhamiaji, wakati wa mchezo wao uliochezwa leo asubuhi kwenye
viwanja vya Chuo Kikuu cha UDOM mjini Dodoma. Katika mchezo huo Habari
ilishinda kwa raundi mbili mfululizo.
Mchezaji
wa timu ya wanawake Kamba ya Uhamiaji, akibebwa kuwekwa pembeni ili
kupatiwa huduma ya kwanza baada ya kuanguka wakati walipoburuzwa na
wenzao wa Habari na kuwavuta mara mbili mfululizo, katika mchezo wao
uliochezwa kwenye Viwanja vya Chuo Kikuu cha UDOM leo asubuhi.
Uhamiaji wanawake wakijaribu kugangamala kuwazuia Habari, lakini waliburuzwa katia mechi hiyo.
*****************************************
Na www.sufianimafoto.com
TIMU
ya Kamba ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Wanawake leo imeibuka na ushindi
wa mezani baada ya timu ya kamba wanawake ya Katiba na Sheria kuingia mitini.
Mwamuzi
wa mchezo huo alipuliza kipyenga na kutoa ushindi huo kwa timu hiyo ya
Ofisi ya Makamu wa Rais, wanawake baada ya kuita timu zote kuingia
uwanjani kwa ajili ya kucheza na kujitokeza timu moja ambayo ilipewa
ushindi wa bure. Kwa ushindi huo sasa timu hiyo ya Wanawake OMR, inatarajia kucheza na timu ya Bunge kesho katika viwanja vya Chuo Kikuu UDOM.
Wakati
wanawake wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakipata ushindi wa chee, wenzao
wanaume pia wameshinda mchezo huo kwa kuwaburuza bila huruma timu ya Katiba na Sheria wanaume, katika raundi zote mbili mfululizo.
Timu
ya Soka ya Ofisi ya Makamu wa Rais inashuka dimbani leo mchana saa nane
kutupa karata yake ya kwanza kwa kukipiga na Mambo ya nje, mchezo utakaochezwa kwenye Viwanja vya Chuo Kikuu cha UDOM, mjini Dodoma.
Akizungumza
na mtandao huu, Kocha wa timu hiyo, Ucheche, alisema kuwa amekiandaa
kikosi chake chenye wachezaji wazoefu waliojipanga kuonyesha soka la ukweli jioni ya leo.
Aidha
aliwataja baadhi ya wachezaji wanaokiwakilisha kikosi chake kuwa ni
pamoja na Jumanne, Mhina, Kihoko, Issa, Sufiani, Lucas, Kifaru, Mandia, Kibik, Mascat na wengineo.
Post a Comment