Waziri mkuu Mizengo Pinda
akisalimiana na mkuu wa shule ya sekondari Weruweru Rosalia Frimini mara
baada ya kuwasili kwa ajili ya shrehe za miaka 50 ya
shule hiyo
Waziri mkuu Mizengo Pinda
akisalimiana na walimu pamoja na viongozi wa shule ya sekondari Weruweru mara
baada ya kuwasili katika shule hiyo kwa ajili ya sherehe za miaka 50
ya shule hiyo
Gwaride la wanafunzi wa kidato
cha tano na sita katika shule ya sekondari Weruweru likipita kwa
heshima mbele ya waziri mkuu Mizengo Pinda wakati wa sherehe za miaka
50 ya shule hiyo.
Gwaride la wanafunzi wa kidato
cha tano na sita katika shule ya sekondari Weruweru likipita kwa
heshima mbele ya waziri mkuu Mizengo Pinda wakati wa sherehe za miaka
50 ya shule hiyo.
Waziri mkuu Mizengo Pinda
akitembelea maonesho mbalimbali yaliyoandaliwa na wanafunzi wa
shule ya sekondari ya Weruweru wakati wa sherehe za miaka 50 ya shule
hiyo.
Waziri mkuu Mizengo Pinda
akitembelea maonesho mbalimbali yaliyoandaliwa na wanafunzi wa
shule ya sekondari ya Weruweru wakati wa sherehe za miaka 50 ya shule
hiyo.
Waziri mkuu Mizengo Pinda
akitembelea maonesho mbalimbali yaliyoandaliwa na wanafunzi wa
shule ya sekondari ya Weruweru wakati wa sherehe za miaka 50 ya shule
hiyo.
Waziri mkuu Mizengo Pinda
akitembelea maonesho mbalimbali yaliyoandaliwa na wanafunzi wa
shule ya sekondari ya Weruweru wakati wa sherehe za miaka 50 ya shule
hiyo.
Waziri mkuu Mizengo Pinda
akikata utepe na kuzindua ukumbi wa mikutano katika shule ya sekondari
Weruweru wakati wa sherehe za miaka 50 ya shule
hiyo.
Waziri Mkuu akiingia
katika ukumbi mpya wa mikutano baada ya kuufungua rasmi
Ukumbi mpya
unavyoonekana.
Waziri mkuu Mizengo Pinda
akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la shule ya sekondari ya
Weruweru.
Mke wa waziri mkuu mama Tunu
Pinda akipanda mti katika eneo la shule ya
wasichana ya Weruweru .
Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda akiwa na Dkt Asha-Rose
Migiro na Dkt Mary Nagu ambao ni baadhi ya kinamama viongozi mashuhuri
waliowahi kusoma hapo
Wana Weruweru wakicheza na kuimba
wakati wa Golden Jubilei ya miaka 50 ya shule
hiyo.
Wana Weruweru wakicheza na kuimba
wakati wa Golden Jubilei ya miaka 50 ya shule
hiyo.
Wana Weruweru wakicheza na kuimba
wakati wa Golden Jubilei ya miaka 50 ya shule
hiyo.
Baadhi ya wageni waalikwa katika
sherehe hiyo.
Baadhi ya wasichana waliomaliza
katika shuel ya sekondari ya Weruweru wakifuatilia matukio mbalimbali
hapa wakiongozwa na Dk Lilian Mtei aliyeshika nyonga. Picha zote na
Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi
PINDA: WANAFUNZI WA ZAMANI KUTANENI NA KUSAIDIA
SHULE MLIZOSOMA
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda
amewataka Watanzania kuiga mfano wa shule ya Sekondari ya Weruweru ambao
wahitimu wake wa zamani (Alumnae) wameamua kuchangisha fedha na kukarabati shule
yao ya zamani.
Ametoa kauli hiyo jana jioni
(Jumamosi, Septemba 21, 2013) wakati akizungumza na mamia ya wanajumuiya
waliohitimu katika shule hiyo (Alumnae), wanafunzi waliopo pamoja na wageni
mbalimbali waliohudhuria sherehe za Jubilei ya miaka 50 ya Shule ya Sekondari ya
Wasichana ya Weruweru.
Waziri Mkuu ambaye alikuwa mgeni
rasmi katika sherehe hizo alisema: “Watanzania wengi tuna nafasi za kuchangia
shule zilizotusomesha. Tuige mfano wa wenzetu wa Weruweru, tukutane na kusaidia
shule tulizosoma,” alisema.
Alisema yeye alisoma sekondari
ya Pugu kati ya mwaka 1965 na 1967 lakini kumekuwa na juhudi mbalimbali za
kuwakutanisha wahitimu wa shule hiyo ambazo hazijawahi kufanikiwa. “Ninawataka
mtembee kifua mbele kwa sababu shule yenu imeza yunda zuri sana,” alisema huku
akiwasifia wana Weruweru waliohitimu zamani kwa kuamua kuja na wazo hilo jema la
kukarabati shule yao ya zamani.
Mapema, akisoma taarifa ya shule
hiyo, Mwalimu Mkuu wa Weruweru, Bibi Rosalia Frimini alisema shule hiyo
iliyoanzishwa Oktoba 22, 1963 hivi sasa ina wanafunzi 570 wa kidato cha tano na
sita tu wanaosoma michepuo ya PCB, EGM,ECA, HGE, HGK na HKL.
Alisema shule hiyo inakabiliwa
na changamoto nyingi ikiwemo uchakavu wa maabara, madarasa, mabweni na mifumo ya
umeme. Alisema shule hiyo ina upungufu wa watumishi wakiwemo manesi, wapishi,
mkutubi na walinzi.
“Shule pia inakabiliwa na tatizo
la usafiri. Landrover 110 iliyopo shuleni ni ya tangu miaka ya 80 na
matengenezo yamekuwa makubwa, tunaomba utusaidie kutatua tatizo la usafiri...
tunapata shida hasa ikitokea watoto wanaumwa na wanatakiwa kupelekwa hospitali
ya mkoa,” alisema.
Akizungumza katika hafla
hiyo, Dk. Maria
Kamm ambaye aliongoza shule hiyo kwa miaka 22 kuanzia mwaka 1970 hadi 1992,
aliiomba Serikali irudishe mfumo wa kidato cha kwanza hadi cha nne kwa shule
kongwe ambao ulifutwa na Serikali. Alisema katika kujenga maadili kwa watoto,
inabidi waanze tangu wanapoingia sekondari.
“Hawa wa kidato cha tano na cha
sita ni wa kupita tu.. umri wa kuumba binti ni kuanzia kidato cha kwanza hadi
cha nne. Tunahitaji kuumba mabinti wa Taifa hili kama ambavyo tulikuwa tukifanya
huko nyuma,” alisema.
Alisema Sera ya Taifa ya Elimu
ya Kujitegemea ilikuwa ndiyo siri kubwa ya kuwaumba wasichana waliopitia shuleni
hapo na kwamba ilileta usawa na kuondoa ubaguzi. “Sera hii ilifanya watoto wote
wawe sawa, iliondoa ubaguzi shuleni kwa sababu wanafunzi wote walijifunza kazi
na kujiamini. Na yote hii ni katika kujenga nidhamu kwa watoto wetu,”
alisema.
“Elimu ya Kujitegemea siyo siasa
kama wengi wanavyodhani, ni jadi ya mwafrika, ni jadi ya mwanamke. Kujitegemea
ndiyo msingi wa maendeleo ya Taifa lolote ulimwenguni, tunaomba Serikali
irudishe elimu ya kujitegemea shuleni ili tuwasaidie watoto wetu.”
Naye Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa
Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro ambaye ni mhitimu wa shule hiyo alisema
Jubilei ya miaka 50 ya Weruweru ni sehemu ya kusherehekea ndoto iliyotimia na
ndoto iliyokuwa kweli kwa wanafunzi wengi waliosoma kwenye shule
hiyo.
“Shule hii ni ya pekee kwa
sababu ilitoa fursa kwa mtoto wa kike pale ambapo hapakuwa na fursa... ilikuwa
ni mchanganyiko wa watoto wa viongozi, wafanyakazi na wakulima”.
Akimnukuu Rais wa zamani wa
China, Mao tse Tung, aliyesema wananwake wanashikilia nusu ya anga, Dk. Migiro
alisema kutokanana usemi huo haiwezekani watu wanaoshikilia nusu ya anga
wakaendelea kubaki nyuma.
Alisema shule hiyo imetoa
wataalamu mbalimbali wakiwemo wanadiplomasia, wanasiasa, viongozi mbalimbali wa
mashirika, taasisi na serikali na pia imetoa rubani wa kwanza mwanamke hapa
nchini.
Baadhi wa wanafunzi waliohitimu
katika shule hiyo ni Dk. Asha-Rose Migiro, Dk. Mary Nagu, Balozi Mwanaidi
Maajar, Bi. Anna Kilango Malecela, Dk. Mwele Malecela, Dk. Hellen Kijo-Bisimba,
Hajat Amina Mrisho na wengine wengi ambao wameshika nafasi mbalimbali za uongozi
katika mashirika, taasisi na Serikalini.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI
MKUU,
JUMAPILI, SEPTEMBA 22,
2013.
Post a Comment