|
Mmoja wa wakazi wa Rugelele kata Rujewa wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya DUKA MKWILA[20]ni miongoni mwa wananchi waliopiga simu za uongo katika kikosi cha zimamoto mkoa wa mbeya akiwa amepewa adahabu ya kuosha gari la zimomoto |
|
Hata hivyo DUKA alikiri kutenda kosa na kuomba msamaha kwa jeshi hilo ambapo aliachiwa huru na kisha kurejea kwao huku akijutia kosa alilolifanya na kuahidi kutorudia tena.
|
|
JESHI la zimamoto na uokoaji limewataka wananchi kuacha matumizi mabaya ya miito ya simu ya dharula kwa Jeshi hilo ili kuepusha usumbufu kwa Jeshi pindi wanapopigiwa simu za dharula.
Wito huo umetolewa na Jeshi hilo baada ya kupata kero za mara kwa mara kutoka kwa wananchi wanaopiga simu kwenye Jeshi hilo wakihitaji huduma za gari hilo lakini wanapofika eneo waliloelekezwa wanakuta hakuna tukio lolote.
Wamekuwa wakipokea simu nyingi za uongo hivyo serikali kuingia gharama kubwa za mafuta ambayo yangetumika kwenye maafa pindi yanapotokea.
Mmoja wa wakazi wa Rugelele kata Rujewa wilaya ya MBARALI DUKA MKWILA[20]ni miongoni mwa wananchi waliopiga simu za uongo katika Jeshi hilo mara kadhaa na kuomba huduma nyingine badala ya ajali ya moto hali iliyofanya Jeshi hilo kumkamata na kumhoji.
DUKA amesema yeye namba hiyo alipewa na mtu mwigine aliyedai kuwa mwenye namba hiyo huwa anatoa pesa za FREE MASON pia dawa za kienyeji kwa matatizo mbalimbali.
Hata hivyo DUKA alikiri kutenda kosa na kuomba msamaha kwa jeshi hilo ambapo aliachiwa huru na kisha kurejea kwao huku akijutia kosa alilolifanya na kuahidi kutorudia tena |
on Monday, September 30, 2013
Post a Comment