Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda akitoa maelezo ya
kuhamishwa kwa kijiji cha Bugwe na kujadili hoja nyingine katika kikao
cha madiwani kwenye ukumbi wa Mikutaano Halmashauri ya Wilaya Mpanda.
Diwani
wa Kata ya Katuma akitoa mafafanuzi kuhusiana na hoja ya kuhamishwa kwa
kijiji cha Bugwe kwa kile kilichodaiwa kuwa kinachangia katika
uharibifu wa mazingira. Kwa waliokaa ni wajumbe wa baraza la madiwani
wakifuatilia hoja ya mwenzao. Madiwani
wa Halmashauri ya wailaya ya Mpanda wakiwa kwenye vikao vyao vya
kawaida vya maamuzi vya Mabaraza kujadili maendeleo ya mstakabali ya
watu wake na Taifa kwa ujumla.
Na Kibada Kibada –Mpanda Katavi.
Baraza
la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kwa kauli moja limepinga
maamuzi ya kukihamisha na pengine kukifuta kabisa Kijiji cha Bugwe
kilichopo katika Kata ya Mpandandogo Wilayani Mpanda kwa kile
kilichoelezwa kuwa kinachangia katika uharibifu wa mazingira.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti kwenye kikao hicho Diwani wa Kata ya Mpandandogo
Hamadi Mapengo,Diwani wa Kata ya Katuma Mhe Msemo,Diwani wa Kata ya
Sibwesa Gaudesi Lusambo, na Diwani wa Viti Maalum Kata ya Mwese Teodora
Kisesa walipinga kuhamishwa kwa kijiji hicho wakidai kuwa walijiridhisha
kuwa wananchi wa kijiji hicho hawahusika katika kuchangia uharibifu wa
mazingira .
Hata
hivy walishauri kuwa watu waliovamia maeneo yasiyoruhusiwa
yaliyotengwa na yale maeneo ya vyanzo vya maji wafugaji waliovamia
maeno hayo kinyume na sheria kutoka mikoa ya Shinyanga kupitia mto
ugala na kuharibibu mazingira kwenye vyanzo vya maji waondolewe kuliko
kuwaondoa wananchi waliokutwa katika kijiji chao na wameishi hapo miaka
mingi na walisajiriwa kisheria..
Kijiji
cha Bugwe ambacho kimesajiliwa mwaka 2011 kina kaya 322 zenye wakazi
wapatao 2049 kati yao wanaume 1044 na wanawake 1005 kwa mjibu ya Sensa
ya watu na makazi ya mwaka 2012 ambapo hata hivyo inadaiwa kuwa wapo
watu wengi ambao hawajahesabiwa katika zoezi hilo la sense hivyo
inakadiliwa kuwa na wakazi wengi zaidi ya idadi iliyolasimi.
Kijiji
hicho cha Bugwe kinadaiwa kuwa kinazunguukwa na mito mingi ambayo ndiyo
tegemeo la wakazi wa wilaya ya Mpanda kutokana na maji yanayotiririka
kutoka kwenye vyanzo vya mito iliyoko kwenye kijiji hico cha Bugwe kama
inavyodaiwa na wataalam wa Idara ya adhi kuwa wananchi wa Bugwe
wanachangia kuharibu mazingira.
Akizungumza
katika kikao hicho Mbunge wa jimbo la Mpanda Vijijini ambaye naye ni
sehemsou ya baraza la madiwani Moshi Selemani Kakoso alikieleza kikao
cha Madiwani kuwa anaungana na maamuzi ya Baraza la Madiwani la kukataa
kukihamisha au kukifuta kijiji cha Bugwe kwa kile kilichoelezwa kuwa
kiko kwenye vyanzo vya maji na kinachangia uharibifu wa mazingira.
Mbunge
huyo alieleza kuwa vyanzo vya maji vinavyozungumziwa viko umbali mrefu
kutoka kijiji kilipo cha Bugwe,na eneo hilo ni moja ya eneo nzuri sana
na ni eneo oevu kutokana na mazingira yake yanaonekana kama yale
yaliyoko hifadhi ya ngorongoro na ni eneo lililoko katikakati ya Tarafa
ya Kabungu na Tarafa ya Mwese.
Na
eneo hilo limevamiwa na wavamizi wafugaji kutoka mikoa ya jirani wakiwa
na mifugo ambayo wanaipitisha mifugo kupitia mto ugalla wakitokea
mikoa ya jirani, na kuvamia maeneo ya vyanzo vya maji ambavyo ni vyanzo
vya mito ya lugufu,katuma,mto mnyamasi,mto lwegele,mfwisi,mto lufilisi
na mto lwega na baadhi ya mito inamwaga maji katika ziwa Tanganyika.
Kikao
kilitoa maamuzi ya kutokukifuta kijiji cha Bugwe badala yake Serikali
ikawaondoe wale wavamizi wa vyanzo vya maji ambao wanaishi kule wakiwa
na makundi makubwa ya mifugo ambayo inachangia uharibifu wa mazingira.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda
Estomih Chang’ah akizungumzia suala la kuhamishwa kwa kijiji cha Bugwe
alieleza kuwa suala hilo liliagizwa na ngazi ya mkoa baada ya kupokea
maagizo kutoka ngazi ya wilaya na lilikuwa limeisha jadiliwa kwenye
ngazi ya Halmashauri.
Mkurugenzi
ameliomba baraza limwagize Mkurugezi awasilisiliane na Katibu Tawala
Mkoa wa Katavi Mhandisi Emanuel Kalobelo iundwe timu ya mkoa wa
itakayoenda huko kuona na kujiridhisha katika maeneo yanayodaiwa kuwa ni
vyanzo vya maji vimevamiwa na wananchi wa Kijiji cha Bugwe.
Kwa
kauli moja Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Yasini
Kibiriti alirithia kwa kauli moja maamuzi ya Kikao cha madiwani kupinga
kuhamisha na kufutwa kwa kijiji cha Bugwe kwa kuwa kufanya hivyo itakuwa
kuwaonea wananchi na watakuwa hawajatendewa haki kwa kuwa hawahusiki
katika uharibifu wa mazingira wao ni rafiki wa kutunza mazingira.
Post a Comment