Mhadhiri
Mwandamizi wa Sheria na Haki za Binadamu kutoka Chuo Kikuu cha DSM,
Bwana James Jesse, ndiye aliyekuwa Mwezeshaji wa mafunzo hayo. Hapa
anaonekena akinukuu michango ya washiriki wa warsha wakati wa
majadiliano ya pamoja.
Naibu
Mkurugenzi wa masuala ya Haki za Binadamu kutoka Ofisi ya Mwanasheria
Mkuu wa Serikali, Bi. Sarah Mwaipopo alikuwa miongoni mwa watoa mada
katika warsha hiyo. Hapa akiwasilisha mada yake kuhusu wajibu wa
Serikali katika utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu nchini.
Mmoja wa washiriki akiwasilisha taarifa ya majadiliano ya kikundi chake wakati wa mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada wakati wa mafunzo hayo.
Wanawarsha wakiteta jambo wakati wa majadiliano ya vikundi.
Maafisa
wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bi. Caroline Kisunte
(kushoto) na Bi. Bitizani Kejo wakifuatilia mada wakati wa warsha hiyo
ya mafunzo.
Mkurugenzi
wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,
Bwana Nabor Assey na Mtaalamu Mshauri wa masuala ya haki za binadamu
kutoka Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa,
Kanda ya Afrika Mashariki, Bi. Meklit Hessebon (katikati) katika picha
ya pamoja na mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo yaliyomalizika jana
jijini Dar.
Washiriki
wa mafunzo kuhusu haki za binadamu na utoaji haki, mahakimu wakazi
kutoka Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro wakiwa katika picha ya
pamoja na maafisa wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB).
Mafunzo hayo ya siku tatu yaliandaliwa na THBUB kwa kushirikiana na
Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa Kanda ya
Afrika Mashariki, Addis Ababa, Ethiopia.
Wakiwa
wenye nyuso za furaha washiriki wa mafunzo ya haki za binadamu na
utoaji haki wakitawanyika kuelekea makwao mara baada ya mafunzo hayo
kuhitimishwa.(Picha zote na Germanus Joseph).
Post a Comment