PIX 1
Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Seth Kamuhanda (katikati) akiwasili Uwanja wa Taifa kuhudhuria hafla ya kumuaga. Kushoto ni Naibu Katibu mpya wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel na kulia ni Katibu Mkuu wa mpya wa Wizara hiyo Bi. Siaba Nkinga.
PIX 4 PIX 4
Viongozi hao wakiwa wakielekea kwenye ukumbi kwa ajili ya kushiriki hafla ya kumuaga aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Seth Kamuhanda (katikati). Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Siaba Nkinga na kushoto ni Naibu wake Profesa Elisante Ole Gabriel.

PIX 3
Katibu Mkuu wa mpya wa Wizara hiyo Bi. Siaba Nkinga (kushoto) akiwa pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Seth Kamuhanda (kulia).
 PIX 5
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi wa hafla hiyo Bw. Seth Kamuhanda iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
PIX 6
Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Seth Kamuhanda akihutubia wakati wa hafla ya kuagwa kwake iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
PIX 7
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bi. Siaba Nkinga akimkabidhi zawadi aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Seth Kamuhanda.
PIX 8
Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Seth Kamuhanda (aliyesimama katikati) akiifurahia zawadi aliyopewa na Katibu Mkuu mpya wa Wizara hiyo katika hafla iliyoandaliwa na Wizara hiyo. Kushoto ni Katibu Mkuu mpya wa Wizara hiyo Bi. Siaba Nkinga na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam
PIX 9
Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Seth Kamuhanda (kushoto) pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel wakiangalia kwa furaha zawadi aliyokabidhiwa Bw. Kamuhanda kwenye hafla ya kuagwa kwake.
PIX 10
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akikabidhiwa zawadi.
PIX 11
 Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Seth Kamuhanda (wa tatu toka kulia mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
PIX 12
Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Seth Kamuhanda (wa nne toka kulia mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Wizara na Wakurugenzi.(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO, DAR ES SALAAM).
Na Eleuteri Mangi.
WAMILIKI  wa vyombo vya habari nchini wameaswa kuwajengea mazingira mazuri waandishi wa habari wa vyombo vyao ili waweze kuhabarisha umma wa Watanzania mambo mbalimbali yanayotokea ndani na nje ya nchi kwa kuzingatia weledi wa taaluma yao.
Rai hiyo imetolewa na Katibu Mkuu aliyemaliza muda wake wa kuitumikia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Seith Kamuhanda jana alipokuwa anaagwa na watumishi wa wizara hiyo katika hafla iliyofanyika kwenye Uwanja wa Michezo wa Taifa jijini Dar es Salaam.
“ Wamiliki wa vyombo vya habari wajenge mazingira mazuri ya kuwawezesha waandishi wa habari kusafiri ndani na hata nje ya nchi. Kwa kufanya hivyo unawapa fursa nzuri ya kujifunza mambo mengi ya kuihabarisha jamii ya Watanzania.
“Mwandishi asiye safari anakuwa na uelewa finyu wa mambo kwani ni jambo la msingi ajue nchi nyingine mambo yanaendaje ili aweze kulinganisha na maendeleo ya nchi yetu,” alisema Kamuhanda.
 Kamuhanda alisema kuwa wamiliki wa vyombo vya habari kuwapa fursa waandishi wa habari kusafiri  hilo ni jukumu lao la kwanza.
Kamuhanda aliongeza kuwa hata yeye alipokuwa mwandishi wa habari alijifunza mambo mengi alipokuwa akisafiri ndani na nje ya nchi, kwani kusafiri kunapanua mawazo na kuwa na uwezo mpana “exposure” wa kupambanua mambo juu ya nini cha kuandika na kuuhabarisha umma kulingana na maadili ya uandishi wa habari. 
Aidha, Kamuhanda aliwaasa wamiliki na waadishi wa habari kuutumia vizuri uhuru wa vyombo vya habari uliopo hapa nchini. Sanjari na hilo, aliviasa vile vinavyokiuka miiko na maadili ya habari na kutumia vibaya uhuru huo vitambue kuwa wote wapo kwa ajili ya kuiletea sifa nzuri nchi yetu.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa sasa wa Wizara hiyo, Sihaba Nkinga amempongeza Katibu Mkuu huyo aliyemaliza muda wake kwa kuitumikia Wizara hiyo kwa uaminifu kwa   kipindi  cha  wa miaka minne.
Sihaba alisema kuwa Wizara anayoiongoza itaenzi kwa kusimamia na kuendeleza mambo aliyoanzisha Kamuhanda ikiwemo kudumisha umoja wa watumishi katika wizara na taasisi zake.
Naye Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni Profesa  Hermans Mwansoko akitoa neno la shukrani kwa Kamuhanda  kwa niaba ya wafanyakazi alisema wizara hiyo  itamkumbuka Kamuhanda kwa mpango wa kuwa na ofisi ya uhakika Dodoma, kuanzisha Bodi ya Filamu, kujali afya na uzima wa watumishi na kujali suala la jinsia katika ngazi za maamuzi ndani ya Wizara.
Kamuhanda alikuwa  Katibu Mkuu wa Wizara hiyo  na kufanya kazi chini ya Mawaziri George Mkuchika, Naibu wake Joel Bendera, Dkt. Emmanuel Nchimbi, Naibu wake Fenella Mkangara.
Hadi mabadiliko ya nafasi za makatibu wakuu yalipotokea   hivi karibuni alifanya kazi chini ya Waziri Fenella Mkangara Naibu wake akiwa Amos Makala.