Mke wa Rais na Mwenyekiti wa
Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa na
Mwanzilishi na Mtendaji mkuu wa Taasisi ya Opportunity Education Bwana Joe
Ricketts kwenye uwanja wa ndege katika mji wa Omaha uliopo katika Jimbo la
Nebraska nchini Marekani
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akipokea ua kutoka kwa binti Kate Stephens, 7, mara baada ya Mama Salma kutua
kwenye uwanja wa ndege wa Omaha katika jimbo la Nebraska nchini
Marekani
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akionyeshwa na Bwana James Ricketts, Rais na Mtendaji Mkuu wa wa Taasisi ya
Oppoturnity Education shughuli mbalimbali za kununua na kusafirisha vifaa vya
elimu kwenda kwenye shule katika nchi mbalimbali hapa duniani ikiwamo Tanzania
wakati Mama Salma alipotembelea Taasisi hiyo yenye Makao Makuu yake huko Omaha
katika Jimbo la Nebraska nchini Marekani
Mwenyekiti wa Taasisi ya
Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akipokea zawadi ya ngao kutoka
kwa Bwana Joe Ricketts, Mwanzilishi na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Opportunity
Education iliyoko huko Omaha nchini Marekani. Bwana Ricketts alitoa zawadi hiyo
kwa kutambua mchango mkubwa sana alioufanya Mama Salma binafsi na Taasisi yake
ya WAMA Foundation katika masuala ya elimu. Afya na uwezeshaji kwa akina
mama..
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa
WAMA, Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na uongozi wa juu wa Taasisi ya
Opportunies Education kwenye ofisi za taasisi hiyo huko Omaha Nebraska nchini
Marekani. Kulia kwake ni katubu wa WAMA Bw. Daudi
Nasibu
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akikaribishwa kwenye Mji Mkuu wa Jimbo la Nebraska, Lincoln, huko Marekani na
Dr. Natalie Hahn, Mwanzilishi wa Malaika Foundation na Mshauri Mwandamizi wa
United Nations Fund for International Partnership (UNFIP)
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akwia kwenye Mji Mkuu wa Jimbo la Nebraska, Lincoln, huko Marekani na Dr.
Natalie Hahn, Mwanzilishi wa Malaika Foundation na Mshauri Mwandamizi wa
United Nations Fund for International Partnership (UNFIP)
.Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akipokewa na Dr. Marjorie Kastelnik, Dean, College of Education and Human
Sciences kwenye Chuo Kikuu cha Nebraska ambapo Mama Salma alishiriki kwenye Gala
to support Global Education kwenye Chuo Kikuu cha Lincoln huko
Nebraska
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akisalimiana na Mke wa Bwana Joe Ricketts kwenye hafla ya Taasisi ya Support
Global Education .
Mke wa Rais Mama Salma
Kikwete akihutubia waalikwa waliohudhuria hafla ya Taasisi ya Support Global
Education iliyoandaliwa kwa ajili ya kumtunuku tuzo maalum Bwana Joe Ricketts
kwa juhudi zake za kuboresha elimu duniani hasa katika nchi
zinazoendelea.
PICHA NA JOHN LUKUWI
Taasisi ya Opportunit
PICHA NA JOHN LUKUWI
Taasisi ya Opportunit y
Education kutoa tablets kwa wanafunzi nchini
Na Anna Nkinda – Maelezo, Lincoln
28/9/2013 Taasisi ya fursa ya Elimu (Opportunity
Education) ya nchini Marekani imeazimia kuanzisha mradi wa laptop ndogo
(tablets computer) kuanzia mwezi Januari mwaka 2014 nchini ambazo zitatumika
kufundishia ili walimu waweze kufundisha haraka na kwa ufanisi zaidi pia
wanafunzi watapata nafasi ya kujifunza zaidi.
Hayo yamesemwa jana na Joe Ricketts ambaye ni mwanzilishi
na mtendaji mkuu wa taasisi hiyo wakati wa hafla ya kuchangia uugwaji mkono wa
utoaji elimu barani Afrika iliyoandaliwa na taasisi ya Malaika ya nchini humo
na kufanyika katika chuo Kikuu cha Nebraska kilichopo mjini Lincoln
.
Ricketts alisema mradi huo kwa mara ya kwanza utaanzia
nchini Tanzania ambapo wanafunzi zaidi ya 1000 kutoka shule 10 tofauti watapewa
laptop ndogo kwa ajili ya kusomea na baada ya kipindi cha mwaka mmoja
watafanya mtihani ili kuangalia tofauti iliyopo kwa wale waliokuwa wakitumia na
wasiotumia.
Baada ya majaribio hayo kama kutakuwa na mafanikio basi
mradi huo utasambazwa katika shule nyingine nchini Tanzania ili kila mwanafunzi
aweze kupata nafasi ya kusoma kwa kutumia laptop hizo na hii itakuwa ni nafasi
kwao ya kuweza kujitunza zaidi.
“Kwa mara ya kwanza nilipokuwa nchini Tanzania
nilipita Serengeti na kukuta mtu anajitahidi kutengeneza nyumba ambayo ni
ngumu kuitengeneza hii inamaana kuwa mwalimu mmoja alikuwa anafundisha wanafunzi
zaidi ya miamoja niliamua kuanzisha mahusiano na shule hiyo ambayo niliwapelekea
vifaa mbalimbali vya kufundishia”.
“Lengo la kuanzishwa kwa Taasisi hii ni kutoa msaada wa
kielimu ikiwa na nia ya kufanya upatikanaji wa elimu bora kwa wanafunzi kutoka
nchi zinazoendelea ili wale wanaotoka katika familia maskini waweze kusoma na
kupata ajira pale watakapokuwa wamemaliza masomo yao na hivyo kujikwamua na hali
ngumu ya maisha”, alisema Ricketts.
Alimalizia kwa kusema kuwa program zao za kufundishia
wanafunzi zimeandaliwa kwa lugha ya kiingreza lakini hivi sasa wameanza kuandaa
program hizo kwa njia ya Kiswahili jambo ambalo litazifanya shule ambazo
zinafundisha kwa lugha hiyo nazo kunufaika na Taasisi hiyo.
Kwa upande wake Mke wa Rais Mama Salma Kikwete aliishukuru
taasisi hiyo kwa kusaidia kuboresha elimu nchini na kuiomba kuangalia uwezekano
wa kuzifikia shule, walimu na wanafunzi waliopo vijijini ambao nao wanahitaji
kupata njenzo nzuri za kufundishia na material mazuri ya kusoma kama ilivyo kwa
wanafunzi wa mjini.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya
Wanawake na Maendeeo (WAMA) alisema kuwa kupitia taasisi hiyo ameweza kuwasaidia
watoto wa kike ambao ni yatima na wanaotoka katika mazingira hatarishi ambao
hawakupata nafasi ya kupata elimu kuwapatia ufadhili wa masomo na hivyo
kuendelea na masomo yao.
Pia ameweza kuinua uchumi wa wanawake jambo ambalo
limewafanya waweze kuimarisha hali zao za maisha kwa kuwapatia elimu ya
ujasiriamali na kuwaongezea mitaji ya vikundi vyao vya
maendeleo.
Mama Kikwete alisema, “Nakupongeza Bwana Ricketts kwa kazi
unayoifanya ya kuzisaidia shule zaidi ya 400 nchini Tanzania msaada unaoutoa wa
vifaa vya kufundishia unawafanya walimu waweze kufundisha masomo yao vizuri
naamini tutajenga mahusiano mazuri kati ya Taasisi yako na WAMA ili kuhakikisha
kuwa program hii inafanikiwa na kutimiza malengo yake”.
Taasisi hiyo ilianzishwa mwaka 2005 na kusajiliwa nchini
mwaka 2006 walianza kufanya kazi na shule moja ya msingi na hadi kufikia
sasa shule 434 zikiwemo za Sekondari 33 zimenufaika kwa kupata vitabu, DVD na
zana za kufundishia.
Kwa upande wa shule za sekondari wanatoa mwongozo wa
mwalimu ambao unamuongoza kirahisi jinsi ya kuwafundisha wanafunzi , laptop
ambazo zinamasomo yaliyorekodiwa ambayo ni ya sayansi, hesabu, kiingereza na
maarifa ya jamii ,projecta na Televisheni ambazo zinasaidia kuonyesha masomo na
vitabu na video inawasaidia wanafunzi kujifunza somo la kiingereza kwa njia ya
kusikiliza na kusoma.
Mama Kikwete alipata nafasi ya kutembelea makao makuu ya
Taasisi hiyo yaliyopo katika mji wa Omaha na kujionea nyenzo mbalimbali za
kufundishia vikiwemo vitabu na DVD zikiwa zimefungwa kwa ajili ya kupelekwa
katika nchi mbalimbali zinazoendelea za bara la Afrika na Asia ikiwemo
Tanzania.
Post a Comment