Mke wa mkuu wa waandishi wa habari
kampuni ya Mwananchi Communication LTD mkoa wa Morogoro, Venance George
(40) Sauda Mgombelwa akilia mara baada ya kuag
a mwili wa mume wake wakati wa misa kabla ya kuanza safari ya kwenda kijiji cha Bukoti Geita kwa mazishi, Venance alifariki dunia Septemba 26 mwaka huu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro ambako alilazwa.
a mwili wa mume wake wakati wa misa kabla ya kuanza safari ya kwenda kijiji cha Bukoti Geita kwa mazishi, Venance alifariki dunia Septemba 26 mwaka huu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro ambako alilazwa.
Venance George enzi za uhai wake.
Mwandishi wa kampuni ya IPPMEDIA mkoa
wa Morogoro Devotha Minja akiwa mwenye huzuni huku akiwa amemkumbatia
Hamida Shariff wa gazeti la Mwananchi Morogoro jana wakati wa kuaga
mwili wa bosi wake.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera
kushoto akimpa pole baba wa Venance George, Mzee George Mhakingilwa
wakati wa misa ya kuaga mwili wa marehemu Venance, Kulia ni Mke wa
Marehemu Sauda Mgombelwa.
Bendera akifafanua jambo huku George
Mhangilwa (katikati) na Boninvetura Mtalimbo kulia wakisikiza jambo muda
mfupi kabla ya kuanza safari ya kusafirisha mwili wa marehemu Venance
George kwenda kijiji cha Bukoti Geita kwa ajili ya mazishi.
Jeneza lenye mwili wa mwaandishi
Venance George likiingizwa katika basi ndogo aina ya coaster tayari kw
kuanza safari..
Mtoto wa kiume wa Venance George, Erasto akiwa amekaa katika gari hilo.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera
akisali na kutoa heshima za mwisho kwa Mwananchi Venance George wakati
wa zoezi la kuaga.
Mratibu wa Morogoro Press Club
Morogoro, Thadei Hafigwa akiweka shada la maua katika jeneza lenye mwili
wa marehemu Venance George na kutoa heshima za mwisho.
Mratibu wa mazishi ya Venance George, Bonveture Mtalimbo akizungumza jambo.
Waandi wa magazeti ya HabariLeo John
Nditi kulia na Peter Kimath JamboLeo wakitoa heshima za mwishi.
Mwandishi wa gazeti la Uhuru na
Mzalendo mkoa wa Morogoro Latifa Ganzel kulia na Ester Mwimbula wa
Mwananci nao wakitoa heshima za mwisho.PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
Dastan Shekidele kulia naye akitoa heshima za mwisho katika tukio la kuaga mwili wa marehemu.
Katekesta wa kanisa la romani katoliki
jimbo la Morogoro Ernest Mathey akinyunyuzia maji ya baraka katika
jeneze lenye mwili wa Venance George nyumbani kwake mtaa wa Tubuyu kata
ya Tungi Manispaa ya Morogoro.PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
Kutoka kushoto, Devotha Minja (ITV)
Hamida Shariff (Mwananchi) Mwenyekiti wa Morogoro Press Club, Idda
Mushi, Latifa Ganzel (Uhuru na Mzalendo) na Lilian Lucas (Mwananchi)
wakifuatilia jambo wakati wa misa ya ibada ya marehemu Venance George
(40) iliyofanyika nyumbani kwake mtaa wa Tubuyu kata ya Tungi Manispaa
ya Morogoro jana.PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
Mtoto wa kwanza wa Veanace George, Ivon Veanace George akiwa mwenye huzuni wakati wa ibada hiyo.
kutoka kushoto mstari wa nyuma, Lilian
Justice (Majira) Amina Saidi (Star Tv) na Merina Robert (Mtanzania na
Clouds Fm) kila mmoja akiwa ameweka pozi la majonzi wakati wa tukio
hilo.
Mwandishi wa Tanzania Daima, Joseph
Malembeka kulia akisaidiana na mwenzake kumpa msaada mwanamke ambaye
aliishiwa nguvu wakati wa tukio la kuaga.PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
Mwenyekiti wa Morogoro Press Club Idda Mushi akitoa neno juu ya msiba huo.
Mwenyekiti wa CCM wilaya Morogoro Fikiri Juma akizungumza jambo
Katibu wa mbunge wa jimbo la Morogoro kupitia CCM, Abdullaziz Abood, Mourice Massala naye akizungumza jambo
Huyu ndiye Andrew Mpasa ambaye ni Meneja Mauzo gazeti la Mwananchi Morogoro akihakikisha kila jambo lina kwenda sawa katika msiba huo.
Timu ya watumishi wa Mwananchi Communication LTD katika msiba huo.
HISTORIA FUPI YA MAREHEMU
VENANCE GEORGE.
Marehemu Venance George
Mhangilwa alizaliwa mnamo 8/12/1973 Bukoti wilaya ya Geita.
ELIMU:
-Marehemu alisoma katika shule
ya msingi Bugogo kuanzia mwaka 1981 mpaka mwaka 1987 alipohitimu elimu yake ya
msingi.
-Mnamo mwaka 1988 alianza kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Forest Hill iliyopo Morogoro na kuhitimu kidato cha sita mnamo mwaka 1994.
-Mnamo mwaka 1988 alianza kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Forest Hill iliyopo Morogoro na kuhitimu kidato cha sita mnamo mwaka 1994.
-Mwaka 1995 alijiunga katika
chuo cha uandishi wa habari na kuhitimu mwaka 1996.
AJIRA:
Marehemu alianza kazi ya uandishi
wa habari katika kampuni ya,
-Uhuru Publication Limited, 1996-1998.
-Kuna Entarprises Company
Limited, 1998-1999.
-Village Travel And Transport
Project (VTTP), 2001-2003.
-Swiss-Contact Tanzania
Limited, 2001-2003
-Mwananchi Communication
Limited, 2003 mpaka mauti yalipomkuta.
Pia alijiendeleza kimasomo
katika chuo kikuu huria cha Tanzania
ambapo alitakiwa kuhitimu shahada yake ya mawasiliano ya umma mwezi wa 12 mwaka
huu 2013.
MWISHO:
-Marehemu alikuwa akisumbuliwa
na vidonda vya tumbo kwa muda mrefu na kifua hali iliyopelekea kwenda kulazwa
katika hospitali ya Aga Khan iliyopo jijini Dar es salaam na kupata nafuu,
Baada ya kurudi nyumbani hali ilbadilika tena na kupelekea kwenda kulazwa
katika hospitali ya Holly Cross Mission iliyopo mkoani Morogoro na baadaYe
kuhamishiwa katika hospitali kuu ya mkoa wa Morogoro.
Marehemu alipata nafuu na kuruhusiwa kurudi nyumbani , baada ya siku kadhaa hali ilibadilika tena na kupelekea kwenda kulazwa hospitali ya mkoa wa Morogoro hadi umauti ulipomkuta mnamo tarehe 26/09/2013 saa 9:15.
Marehemu alipata nafuu na kuruhusiwa kurudi nyumbani , baada ya siku kadhaa hali ilibadilika tena na kupelekea kwenda kulazwa hospitali ya mkoa wa Morogoro hadi umauti ulipomkuta mnamo tarehe 26/09/2013 saa 9:15.
-Marehemu ameacha mjane na
watoto wawili wa kike na wa kiume.
SHUKRANI:
-Tunatoa
shukrani zetu za dhati
kwa wale wote waliokuwa pamoja na sisi tangu marehemu alipoanza kuugua
mpaka
leo hii , shukrani ziwafikie wafanyakazi wenzake, ndugu, jamaa na
marafiki wa karibu. Maelezo haya kwa mujibu wa Mratibu wa mazishia,
Bonveture Mtalimbo.
Post a Comment