VYAMA vitatu vya upinzani nchini vinavyoshirikiana katika harakati za
kupigania katiba mpya, vimebainisha kwamba ushirikiano wao huo utaisha
baada ya kupatikana kwa katiba mpya. Hayo yamebainishwa baada ya kuwapo
fununu kwamba ushirikiano huo utadumu hadi katika uchaguzi mkuu wa mwaka
2015, katika kuking’oa Chama Cha Mapinduzi (CCM) madarakani.
Vyama hivyo vya NCCR-Mageuzi, Chama cha Wananchi (CUF) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), vimesema kwa sasa ushirikiano wao ni kwenye suala la katiba pekee na hayo mengine yatakuja baadaye.
Akizungumza na MTANZANIA Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharrif Hamad alisema kwa kifupi: “ushirikiano ni wa kupigania katiba tu, baada ya hapo hakuna kitu.”
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema kwa sasa ajenda ni katiba mpya pekee.
“Kwa sasa tumelenga fikra zetu katika katiba ili tuweze kupata katiba bora kwani bila misingi mizuri ya demokrasia hatuwezi kufika mbali.
“Nia yetu ni ule mchakato wenyewe wenye maudhui na muafaka wa kitaifa, tusiharibu kwa sasa, hayo mengine ya kushirikaiana katika uchaguzi huenda yakaja baadaye,” alisema Profesa Lipumba.
Naye Katibu Mwenezi wa Chadema, John Mnyika, alisema ushirikiano wa vyama hivyo huenda usiishie hapo watafikiria kuungana katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Hata hivyo, alisema ni mapema mno kuzungumzia suala hilo kwani kipaumbele kwa sasa ni katiba mpya, ila hayo mengine ni kutafakari.
“Jambo kubwa kwa sasa ni kunusuru katiba ambayo imeporwa na CCM, tutaendelea na ratiba yetu ya kukutana na makundi katika jamii na wadau wote na leo (juzi) viongozi wote wako Zanzibar na wakirudi tutaenda mikoani.
“Lengo letu ni kunusuru mchakato wa katiba mpya na mwelekeo wa katiba nchini, tukiruhusu wanayotaka CCM Tanzania itakua kama ya zamani ambapo uchaguzi haukuwa huru na wa haki,” alisema Mnyika.
Wakati huo huo, wasomi nchini wameukosoa ‘utatu mtakatifu’ huo kuwa ni mkakati ambao hauna maandalizi wala mashiko kwa Watanzania.
Kwa nyakati tofauti wasomi hao wamesema mchakato huo haukushirikisha wananchi tangu awali na kitendo cha kuwashirikisha katika hatua ya sasa ni kuwashtua.

Post a Comment