SERIKALI imesema kuwa mpaka ifikapo mwaka 2015 asilimia 30 ya watanzania
waishio vijijini watakuwa wamepata huduma ya umeme kwani kwa sasa
asilimia saba tu ya wananchi waishio vijijini ndio wanapata huduma hiyo
ya umeme.
Kauli hiyo imetolewa jana (leo) jijini hapa na Naibu waziri wa Nishati na madini hapa nchini Steven Massele wakati akiongea na wadau wa mashirika yazilishayo umeme katika nchi za kusini mwa jangwa la sahara(PIESA).
Masele alisema kuwa asilimia 21 ya watanzania ndio wanapata huduma ya umeme ambapo kati yao asilimia saba ndio wanaishi vijiijini lakini kupitia mpango wa wakala wa umeme Vijijini (REA)watahakikisha wilaya
zote na vijiji vyote vinapata umeme kwani ni haki yao ya msingi.
“Tunataka kuona kuwa kila familia hata kama ni ya kijijini inapata umeme na pia kama watapata umeme ni wazi kuwa hata maendeleo yatakuja kwa haraka tofauti na pale ambapo hakuna umeme wala huduma hizo”alisema Masele
Katika hatua nyimgine aliwataka wakala wa umeme vijijini kuhakikisha kuwa wafanya kazi kwa haraka sana ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto ambazo zipo kijijini kwani asilimia kubwa ya wananchi wa vijijini bado hawajaweza kupata huduma hiyo ya umeme lakini pia hawajatambua umuhimu wake.

Awali mwenyekiti wa PIESA ambaye pia ni Kaimu mkurugenzi wa shirika la Tanesco hapa nchini Mhandisi Felchesmi Mramba alidai kuwa lengo halisi la kukutana maeneo hayo ni pamoja na kuhakikisha kuwa wanajadili namna ya kutumia matumizi ya Teknolojia katika kupata umeme
Mhandisi Mramba alidai kuwa kama watafanya hivyo basi wataweza kuruhusu kwa kiwango kikubwa sana upatikanaji wa umeme hasa maeneo ya Vijijini lakini pia kuangalia namna ya matokeo ya tafiti ambazo walizifanya na nchi zilizoendelea Duniani.
Ametaja nchi ambazo zitajadili namna ya upatikanaji wa umeme hasa vijiijini kuwa ni pamoja na Marekani, Mexico,Ausralia, India, Canada,
China, Indonesia,Japani,Kenya ,Malawi Uganda, Botswana , Lesotho pamoja na Afrika ya kusini.
Post a Comment