JAMHURI YA MUUNGANO
WA TANZANIA
WIZARA
YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Simu: +255-22-2112035/40
|
S.L.P. 9223
|
|
Nukushi: +255-2122617/2120486
Barua Pepe: ps@moha.go.tz
|
Dar es Salaam
Septemba
19,2013
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Operesheni Kimbunga haikulenga kuondoa
wahamiaji haramu kutoka Taifa moja
Operesheni
Kimbunga inayoendelea katika mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita hailengi kuondoa
wahamiaji haramu kutoka taifa moja na hadi Septemba 20, 2013, imefanikiwa
kuwakamata watuhumiwa 9,283 toka nchi za Rwanda, Burundi, Uganda, Somalia, DRC
Congo, Yemen na India.
Idadi
kubwa ya wahamiaji hawa haramu
waliokamatwa ni kutoka Burundi (5,355)
wakiafuatiwa na Rwanda (2,379), Uganda (939), DRC Congo (564), Somalia (44),
Yemen (1) na India (1).
Takwimu
zinaonyesha kuwa mkoa wa Kigoma unaongoza kwa idadi kubwa ya wahamiaji haramu
waliondoshwa nchini ikiwa na jumla ya wahamiaji haramu (4,365) ukifuatiwa na
mkoa wa Kagera wenye ambapo walikamatwa wahamiaji haramu (4,335) na Geita (583).
Operesheni
Kimbunga ilianzishwa kwa lengo la
kukabiliana na vitendo vya uhalifu vilivyokithiri vikiwemo ujambazi wa kutumia
silaha,ujangili, utekaji wa magari na mauaji ya kikatili pamoja na migogoro ya
ardhi inayotokana na wafuagaji kutoka nchi jirani kuingiza mifugo yao kwa ajili
ya malisho.
Aidha, jumla ya wahamiaji haramu 3,238 waliondoshwa nchini kwa amri ya
Mahakama baada ya kupewa hati ya kufukuzwa nchini wakati wananchi wengine 1,108
waliokuwa wanachunguzwa kama kweli ni raia wa Tanzania waliachiwa huru baada ya
watendaji kuthibitisha kuwa ni raia halali wakati huo huo wengine 1,303 wakiwa
wanaendelea na uchunguzi ili kuthibitisha uraia wao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Jakaya
Mrisho Kikwete Julai 29, 2013 aliagiza kufanyika kwa opereheni maalum ya
kuondoa uhalifu katika mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita mbao kwa kiasi kikubwa
umechangiwa na kuwepo kwa wahamiaji haramu kutoka nchi jirani.
Operesheni Kimbunga inayoongozwa na Brigedia Jenerali Mathew
Sukambi imeanza rasmi Septemba 6, 2013 baada ya kutoa muda wa wiki mbili kwa
wahamiaji wanaoishi nchini bila kufuata sheria kuondoka kwa hiari yao au
kuhalalisha ukaazi wao nchini.
Taarifa hii imetolewa na Zamaradi Kawawa,
Kiongozi wa Timu ya Habari na Mawasiliano ya Operesheni Kimbunga, Septemba
20,2013, Biharamulo, Kagera.
Post a Comment