JAMHURI YA MUUNGANO
WA TANZANIA
WIZARA
YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
|
|
|
Simu: +255-22-2112035/40
|
S.L.P. 9223
|
|
Nukushi: +255-2122617/2120486
Barua Pepe: ps@moha.go.tz
|
Dar es Salaam
Septemba
19,2013
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Operesheni Kimbunga
Haikuondoa Wakimbizi Nchini
Operesheni Kimbunga haikuondoa Wakimbizi nchini kama
ilivyoripotiwa na baaadhi ya Vombo vya Habari vya hapa nchini na vya nje.
Ifahamike kuwa zoezi hili limehusisha Shirika la Kuwahudumia
Wakimbizi Duniani (UNHCR) ili kuhakikisha kuwa wakimbizi hawahusishwi katika
zoezi la kuondoshwa nchini.
Kwa mujibu wa tafsiri iliyotolewa na Mkataba wa Kimataifa wa
mwaka 1951 kuhusu hadhi ya Wakimbizi, Mkimbizi ni mtu anayekimbia nchi yake kwa
hofu ya maisha yake kuwa hatarini kwa sababu za kikabila, dini, utaifa, uanachama wa chama cha
kijamii au kisiasa na kufuata hifadhi katika nchi nyingine.
Mkimbizi anapokimbilia
katika nchini nyingine kuomba hifadhi ana haki ya kupewa hifadhi na
kuhakikishiwa usalama wake. Pia ana haki ya kupokelewa na kutorudishwa katika
nchi ambayo ameikimbia.
Hivyo , kutokana na Mkataba huo, Tanzania wakati inatekeleza
Operesheni Kimbunga haikumgusa mkimbizi.
Aidha, ieleweke kuwa yapo mazingira ambapo hadhi ya mkimbizi
hukoma pale ambapo suluhisho la kudumu la matatizo ambayo yalimfanya mkimbizi
kukimbia nchi yake limepatikana na hivyo mkimbizi mwenyewe kutaka kurudi nchini
kwake kwa hiari ama pale mkimbizi anapohamishiwa kwenye nchi ya Tatu kwa
makubaliano maalum na pale ambapo mkimbizi anapewa uraia au ukaazi wa nchi iliyompatia hifadhi.
Hivyo basi, mkimbizi anaweza kuwa mhamiaji haramu pale ambapo
hakurudi katika nchi yake kwa hiari baada ya kupatikana suluhisho kwa matatizo
yaliyosababisha kukimbia ama hakupata fursa ya kwenda nchi ya Tatu na hakuomba
Uraia au ukaazi wan chi iliyokuwa inampa hifadhi.
Ieleweke kuwa Mkimbizi ambaye alirudi nchini kwake kwa hiari
yake na baadaye kuamua kurudi katika nchi iliyokuwa inamhifadhi hawezi
kuendelea kuwa na hadhi ile ile ya ukimbizi . Mtu huyu anatakiwa kufuata Sheria
ya Uhamiaji namba 7 ya 1995. Iwapo ataishi nchini bila kufuata sheria hiyo
atahesabika kuwa mhamiaji haramu.
Inawezekana kuna watu ambao hadhi yao ya ukimbizi imekoma na
wanaishi nchini isivyo halali wakakumbwa na
Operesheni Kimbunga na kudai kuwa wao
ni wakimbizi.
Juhudi za Serikali za kuwataka wahamiaji haramu kuhalalisha ukaazi
nchini kwa hiari
Kwa vipindi tofauti, Serikali kupitia Idara ya Uhamiaji
iliendesha zoezi la kuhamasisha watu wanaoishi nchini isivyo halali kurudi
nchini kwao kutokana na hali ya usalama katika nchi hizo kuimarika. Aidha, kwa
waliotaka kubaki na kuendelea kuishi
nchini walielekezwa kufuata sheria na taratibu za Uhamiaji.
Utafiti uliofanywa na Mradi wa Kimataifa wa kushughulikia
masuala ya kiuhamiaji ya Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam unaoongozwa na Prof. Boneventure Rutinwa 2006/2007 katika mkoa wa Kagera unaonyesha kuwa Wilaya ya Karagwe pekee
Inakadiriwa kuwa na wahamiaji haramu 30,850 lakini pamoja na kuhamasishwa
kuhalalisha ukaazi wao, watu 2,000 pekee walifuata taratibu walizoelekezwa na
Maafisa wa Idara ya Uhamiaji ili kuhalalisha ukaaji wao nchini.
Pamoja na juhudi zote za Serikali za kuhamasiha wahamiaji
haramu kuhalalisha ukaazi wao nchini bado hawakufuata taratibu na badala yake
utafiti unaonyesha kuwa waliendelea kuingia na kuhamia katika wilaya nyingine
mfano Biharamulo na maeneo mengine.
Taarifa
hii imetolewa na Zamaradi Kawawa, Kiongozi wa Timu ya Habari na Mawasiliano ya
Operesheni Kimbunga, Septemba 20,2013, Biharamulo, Kagera
Post a Comment