Mtangazaji mahiri wa vipindi vya redio nchini Kenya ambaye alikuwa akitangaza kituo cha redio cha Kiss 100 nchini Kenya, Ruhila Adatia Sood, alikuwa miongoni mwa wahanga walioshambuliwa na wanamgambo wa kikosi cha Al Shabab katika eneo la westgate Mall nchini Kenya.
Kwa muujibu wa taarifa zinaeleza kwamba Ruhila alikuwa ni mjamzito wa miezi sita alipatwa na majereha kadhaa mwilini mwake baada ya kushambuliwa na Al Shabab na kukimbizwa katika hospitali ya Aga Khan iliyopo nchini Kenya kwa ajili ya matibabu na hatimaye kufariki dunia.
Hizi ni baadhi ya vituo vya utangazaji alivyowahi kufanya navyo kazi East Fm, Kiss 100, Kiss TV na XFM.
Hii ndio Picha ya mwisho aliyopiga mtangazaji Ruhila Adatia muda mchache kabla ya kutokea kwa kifo chake alipokuwa akitangaza kipindi cha children’s cooking katika ghorofa ya juu zilizopo studio za East Fm ndani ya Westgate Mall na baada ya hapo alipost zaidi ya picha 8 kupitia mtandao wa Instagram na baadhi ya Tweets mpaka pale taarifa zilivyosambaa kwamba mtangazaji huyo nae ameshambuliwa na Al shabab.
Unaambiwa hizi ni baadhi ya picha za mwisho alizopost Ruhila kupitia mtandao wa Instagram muda mfupi kabla ya kutokea kwa kifo chake.
Chini ni baadhi ya Tweets za watu maarufu na mashuhuri wa Kenya na sehemu mbalimbali wakitoa salamu za pole kwa familia ya mtangazaji huyo.
Post a Comment