Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Muhammed
Shein akikata utepe kuzindua Jengo jipya la kituo cha Jamii na watoto
cha (ZAPHA+) (kushoto) Mwenyekiti wa Bodi ya wazamini wa kituo hicho Bi.
Hasina Hamadi. Welezo nnje kidogo ya Mji Zanzibar.
Baadhi ya
wageni walikwa waliofika katika uzinduzi wa Jengo la kituo cha Jamii na
watoto cha (ZAPHA+) Welezo nnje kidoga ya Mjini Zanzibar.(P.T)
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Muhammed Shein
akiwahutubia wananchi katika uzindizi wa Jengo la (ZAPHA+) huko Welezo
nnje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Wasanii wa
(ZAPHA+) wakionesha igizo jinsi ya watu wenye UKIMWI wanavyo fanyiwa
unyanyapaa,huko Welezo katika uzinduzi wa Jengo la kituo cha Jamii na
watoto cha (ZAPHA+) Mjini nnje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Muhammed Shein
akipata maelezo kwa mshauri Nasaha wa kituo cha (ZAPHA+) Salum Ramadhan
Wakili alipokuwa akiangalia baadhi ya huduma zinazo tolewa kituoni hapo.
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Muhammed Shein
katika picha ya pamoja na watoto wanaopatiwa huduma na (ZAPHA+) huko
kituoni kwao Welezo nnje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
(PICHA ZOTE NA MAKAME MSHENGA WA MAELEZO ZANZIBAR).
Khadija khamis na Riziki Salum Maelezo Zanzibar 22/09/2013.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein amewapongeza viongozi wa ZAPHA +
kwa jitihada zao zilizowawezesha kumiliki jengo lao endelevu la kuweza
kutoa huduma bora kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu pamoja na
watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI Zanzibar.Kauli hiyo alitolewa jana huko katika sherehe za uzinduzi wa jengo jipya la ZAPHA+ Kituo cha jamii na watoto kilichopo Welezo wilaya ya Mjini Magharibi.
Alisema kuwa hatua hiyo iliyofikia ni nzuri na ya kupongezwa kwa mafanikio hayo kwani ni chachu ya maendeleo kwa wanaoishi na maambukizo ya virusi vya UKIMWI katika kujiona wanajamii kuwa na chuo chao cha kupata elimu na ushauri nasaha pia ni chimbuko la matumaini kwa watoto wanaoishi na maambukizi ya UKIMWI.
"Serikali inathamini juhudi zenu za jumuiya kwani inatoa mashirikiano ya pamoja kwa kupiga vita unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na ukimwi," alisema Dkt Shein.
Aidha alisema kuwa zaidi ya watoto 547 tayari waneripotiwa wanaishi na virusi vya ukimwi sawa na asilimia 68 % wakiwa wanaume 194 na wanawake 180 ambao tayari wanatumia dawa za ARV Zanzibar.
Alisisitiza kuwa iko haja ya wananchi kujitokeza kwa wingi katika kushirikiana katika kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu, mayatima na wanaoishi na virusi .
Alisema kuwa iko haja kwa wananchi kukubali kubadili tabia zao na kurudi katika tamaduni zao za mila silka na itikadi za kizanzibari kuweza kupendana kushirikiana na kusaidiana kwa hali na mali .
Aliengezea kuwa wananchi katika kushikamana tupige vita juu ya utumiaji madawa ya kulevya kwani tathmini inaonyesha kuwa asilimia kubwa ya walioathirika ni vijana ambao wamejihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya .
Nae Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Consolata John alisema kuwa amemshukuru Mgeni Rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein kwa kuweza kukubali mwaliko wao kwani ni ishara tosha ya kuwajali na kuwathamini sana mchango wao katika maendeleo ya jamii ya Zanzibar.
Aidha alisema kuwa juhudi kubwa zinachukuliwa katika kuendeleza jumuiya hiyo kwa kuanzisha miradi mbalimabli ya kimaendeleo ikiwemo kilimo cha mboga mboga , utengenezaji wa sabuni na mafunzo ya mapishi kwa watu wanaishi na virusi vya ukimwi.
Jumuiya ya ZAPHA + Zanzibar imeanzishwa mwaka 1994 na kusajiliwa rasmi kama asasi ya kiraiya mwaka 1996 ikiwa na wanachama waanzilishi 26 hadi sasa ina wanachama 2022.
...... MWISHO......
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR .
Post a Comment