Na Mwandishi Wetu, Handeni
SERIKALI kwa kupitia Mkurugenzi
Mtendaji wilayani Handeni, mkoani Tanga, Dr Khalfany Haule, imebariki kufanyika
kwa tamasha la utamaduni la Handeni Kwetu 2013, linalotarajiwa kufanyika
Desemba 14 mwaka huu wilayani humo.
Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ya Handeni, Dr Khalfany Haule, pichani.
Tamasha hilo linafanyika kwa mara ya kwanza wilayani humo likiwa na lengo la kukuza na kutangaza utamaduni na utalii wa Tanzania, ukiwa ni mpango wenye mashiko kwa sekta hiyo.
Tamasha hilo linafanyika kwa mara ya kwanza wilayani humo likiwa na lengo la kukuza na kutangaza utamaduni na utalii wa Tanzania, ukiwa ni mpango wenye mashiko kwa sekta hiyo.
Akizungumza juzi mjini hapa,
Dr Haule alisema ni kitendo kinachopaswa kuungwa mkono na serikali yote
ili kuongeza kasi ya kuleta maendeleo kwa kupitia njia mbalimbali.
Alisema wao kama wilaya
wamepokea kwa mikono miwili wazo zuri la kuandaliwa kwa tamasha hilo wilayani
Handeni mkoani Tanga, hivyo watakuwa pamoja na waandaaji.
“Tunashukuru kwa dhati kuona
mwaka huu mwishoni kunafanyika tamasha hili lenye mguso wa aina yake, maana
watu watakutana kuangalia mambo ya utamaduni wa Handeni na Tanzania kwa ujumla.
“Tupo tayari kushirikiana kwa
karibu na waandaaji wa tamasha hili ili lifanyike kwa mafanikio na kuleta ari
mpya katika sekta ya maendeleo ya Taifa, hususan wilayani Handeni,” alisema
Haule.
Tamasha la Utamaduni wa Handeni
linafanyika kwa mara ya kwanza kwa kuandaliwa na Raha Company And Entertainment likiwa na malengo ya kukuza na kutangaza sekta
ya utamaduni na utalii hapa nchini na kusubiriwa kwa hamu wilayani humo.
Post a Comment