JAMHURI YA MUUNGANO
WA TANZANIA
WIZARA
YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
|
|
|
Simu: +255-22-2112035/40
|
S.L.P. 9223
|
|
Nukushi: +255-2122617/2120486
Barua
Pepe: ps@moha.go.tz
|
Dar
es Salaam
Septemba 19,2013
|
Operesheni Kimbunga na
usakaji wahalifu katika mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Julai 29, 2013
aliagiza kufanyika operesheni maalum iliyopewa jina la Operesheni Kimbunga yenye lengo la kuondoa uhalifu katika mikoa
ya Kagera, Kigoma na Geita ambao kwa kiasi kikubwa umechangiwa na kuwepo kwa
wahamiaji haramu kutoka nchi jirani.
Operesheni
hii pamoja na kufanikiwa kuondosha nchini kwa lazima jumla ya wahamiaji haramu
7,819 kuanzia Septemba 6, 2013 hadi kufikia Septemba 17, 2013, imeweza kushughulikia uhalifu na kufanikiwa
kukamata majambazi wa kutumia silaha, majangili, mabomu ya kutupwa kwa mkono ,
bunduki za aina mbali mbali, Risasi, mitambo ya kutengeneza bunduki aina ya
magobole, Sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania, na kibuyu cha maji cha Jeshi
hilo.
Jumla ya watuhumiwa wa ujambazi wa kutumia
silaha 55 pamoja na mabomu ya kutupwa kwa mkono (8), silaha 47 zikiwemo bunduki
aina ya SMG( 4), Shot gun (4), Bunduki aina ya Riffle (2), Bunduki aina ya Mark
IV (1), Bunduki aina ya Gobole (37) zimekamatwa wakati wa operesheni Kimbunga
hadi kufikia Septemba 17,2013 katika mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita.
Aidha, risasi (602) zilikamatwa zikiwemo Risasi
(500) za bunduki ya aina ya SMG na SAR, Risasi (20) za bunduki aina ya Mark IV
na risasi (82) za bunduki aina ya Gobole, fataki (8), mitambo ya kutengeneza
magobole (2), misumeno ya kukata miti ( 9), Mbao (1,516), Magogo (86), na mkaa
magunia (111).
Aidha,
Watendaji wa Operesheni Kimbunga pia wamefanikiwa kukamata jumla ya majangili
Watanzania (3), Vipande vya meno ya Tembo (2), Ngozi za wanyama mbali mbali
wakiwemo Nyati (1), Duma (1) na Swala
(2). Pia walikamata nyama ya porini,
magunia ya bangi (6), Gongo lita
(86) na lami mapipa (10).
Wakati huo huo, Ng’ombe 3,436
wamekamatwa baada ya wafugaji
haramu kutelekeza mifugo hiyo wakati walipozingirwa na timu ya operesheni
kimbunga katika mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita.
Kumekuwepo
na tabia ya baadhi ya wamiliki wa mifugo kutoka nchi jirani ambao wengi wao ni
matajiri na viongozi serikalini kuwatuma watumishi wao kuingiza mifugo katika
ardhi ya Tanzania hususan kwenye hifadhi ya Taifa kwa ajili ya malisho na
watumishi hao hupewa silaha kwa ajili ya kujihami wakiwa kazini.
Mifugo
imekuwa ikiharibu mazingira na kuleta migogoro ya ardhi katika mikoa hii.
Operesheni
Kimbunga itahakikisha inawakamata wahalifu wote wanaotishia amani hususan
katika mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita.
Aidha,
wananchi ambao ni raia pamoja na Raia wenye asili ya nchi jirani wanaowakaribisha
na kuwahifadhi wahalifu na wahamiaji haramu watakamatwa na kufikishwa kwenye
vyombo vya sheria.
Mhamiaji
haramu ni raia yeyote wa kigeni aliyeingia na kuishi nchini bila kufuata utaratibu uliowekwa na Sheria ya Uhamiaji namba 7 ya mwaka 1995.
Utaratibu
chini ya Sheria hiyo unamtaka raia wa kigeni anayeingia nchini kuwa na Hati ya
kusafiri, kuripoti katika vituo halali vya kuingilia nchini na kujaza fomu za
uhamiaji za kuingia nchini.
Aidha, Raia
wa kigeni anayehitaji kuishi nchini analazimika kuwa na hati za ukaazi
itakayomruhusu kufanya shughuli iliyomleta mfano biashara, matembezi, uwekezaji, Kusoma, matibau,
kufanyakazi nakadhalika.
Operesheni
Kimbunga inayoongozwa na Brigedia Jenerali Mathew Sukambi imeanza rasmi
Septemba 6, 2013 baada ya kutoa muda wa wiki Mbili kwa wahamiaji wanaoishi
nchini bila kufuata sheria kuondoka kwa hiari.
Post a Comment