Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

SERIKALI YAFUTA VIBALI VYOTE VYA UINGIZWAJI WA KEMIKALI

 


Serikali imefuta vibali vya kuingiza kemikali nchini.
Serikali imefuta vibali vya kuingiza kemikali nchini ikiwa ni moja ya hatua za kudhibiti matumizi ya kiuhalifu na kutishia maisha ya wananchi.
Aidha, hatua hiyo imechukuliwa baada ya kuwapo kwa matukio ya mara kwa mara kwa wananchi kumwagiwa tindikali.
Kemikali Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele, alitangaza hatua hiyo juzi  wakati akizungumza  na Dawati la Mkoa la Ukatili wa Kijinsia ofisi  ya Mganga Mkuu wa Mkoa katika warsha iliyolenga  kutoa  elimu juu ya umuhimu wa kumtumia Mkemia Mkuu.
Profesa Manyele alisema kuwa serikali inaendelea kupambana na uingizaji holela wa kemikali ambao ndiyo chanzo cha kubadili matumizi yake na kuangamiza maisha ya wananchi.
Alisema kuwa tatizo kubwa walilolipata ni kutokana na waingizaji, wasafirishaji, watumiaji kubadili matumizi ya kemikali hizo na kuzifanya sehemu ya silaha za kuangamiza wananchi.
Profesa Manyele ambaye yupo katika ziara ya siku sita mkoani, alisema kuanzia sasa wanaohitaji vibali hivyo watalazimika kuomba upya.
 

CHANZO: NIPASHE
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top