Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge Mhe. William V.
Lukuvi amewaeleza wakala wa Hifadhi ya Chakula NFRA kuzingatia ubora na
usafi wa ununuzi wa mahindi kwani mahindi yanayonunuliwa na Serikali ni
kwa ajili ya Chakula.
Alisema
hayo jana wakati wa Ziara yake ya ukaguzi wa vituo vya Mahindi vya
Mtenga, Namanyere na Kasu vilivyopo Katika Wilaya ya Nkasi alipokuwa
akipokea taarifa ya Ununuzi wa Mahindi katika vituo hivyo. Waziri Lukuvi
alisema “itakuwa sio vizuri kununua mahindi ambayo yako chini ya
kiwango na yaliyo na uchafu mwingi kwakuwa
Serikali inanunua mahindi kwa ajili ya matumizi ya chakula ni
sivinginevyo, hivyo lazima Mahindi haya yawe masafi na yenge viwango
bora kwa walaji”.
“Mwaka
huu Serikali imetoa bei nzuri ya Ununuzi wa Mahindi ya shilingi Mia
Tano kwa kilo kwa kuzingatia uhitaji, kutokana na bei hiyo Wakala wa
Hifadhi ya Taifa ya Chakula NFRA inatakiwa kununua mahindi yaliyo safi
ili kuweza kupanga viwango tofauti ambavyo vitawasaidia katika uuzaji wa
Mahindi hayo kwa watu wengine. Kwa kupanga kupanga hovyo Wakala wa
Hifadhi ya Chakula ya Taifa watapata wanunuzi wazuri, alisema Waziri
Lukuvi”.
Alisisitiza
kuwa kwa mwaka huu Serikali ndiyo mnunuzi mkubwa wa Mahindi katika
Kanda zote Tanzania na Wakala wa Hifadhi ya Chakula ya NFRA ndiyo
inayoongoza, katika ununuzi huo ambapo ameagiza NFRA kuanza haraka
usafirishaji wa mahindi kwenda Mkoa wa Shinyanga mapema kabla kipindi
cha mvua hakijaanza.
Akipokea
taarifa ya ununuzi katika kituo cha Kasu, Waziri Lukuvi alielezwa kuwa
kituo hicho kilipanga kununua Tani za Mahindi elfu 2000 hadi kufikia
Mwezi Septemba,2013 hadi sasa kituo hicho kimeshanunua Tani 1,904 zenye
thamani ya shilingi milioni 952,483,500 na kitaendelea na ununuzi hadi
kufikia malengo ya Ununuzi wa Tani zilipangwa.
Akikamilisha
ziara katika Mkoa wa Katavi, Waziri Lukuvi aliwapongeza wananchi wa
Mkoa wa Katavi kwa jitihada zao za kilimo walizozionesha na
kuwahakikishia kuwa katika kila msimu watalipwa fedha zao kwa wakati ili
waweze kuendelea na kazi, pia ameielekeza NFRA kuhakikisha kuwa kila
vibarua wanapomaliza kufanyakazi walipwe ili kupunguza madeni, NFRA
ihakikishe kuwa kila vibarua wanapomaliza kazi zao walipwe mara moja
wasisumbuliwe kwani fedha wanazopata zinawasaidia kuendesha maisha yao
ya kila siku.
Post a Comment