ALIYEKUWA
Mkurugenzi wa Masoko na Fedha Benki Kuu (BoT), Kessinsia Mbatia, amedai
mchakato wa kuipata Kampuni ya M/S Alex Stewart na kuingia nayo mkataba
ulifanywa na Benki Kuu kwa kuongozwa na aliyekuwa Gavana, marehemu
Daudi Balali.
Mbatia alidai hayo jana, alipokuwa akitoa ushahidi wa kumtetea aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Mramba, anayekabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni 11.7 kwa kutoa msamaha wa kodi kwa kampuni hiyo ya ukaguzi wa dhahabu.
Akitoa ushahidi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mjini Dar es Salaam jana, mbele ya jopo la majaji, John Utamwa, Jaji Sam Rumanyika na Msajili Saul Kinemela, alidai mwishoni mwa mwaka 2002, alishughulikia mchakato wa kuipata kampuni ya ukaguzi wa dhahabu kwa kuagizwa na aliyekuwa Gavana wa BoT, marehemu Balali.
“Maagizo niliyopewa na mwajiri wangu ni kuisimamia kamati inayofanya mchakato ili apatikane mkaguzi kwa ajili ya kuisaidia Serikali kujua thamani ya dhahabu inayopatikana, alinikabidhi na watu walioteuliwa kuwemo katika kamati hiyo.
“Wajumbe wa kamati walitoka Wizara ya Nishati na Madini, maofisa wawili kutoka BoT na Mshauri wa Gavana ambaye alihusika kuchambua zabuni za kampuni 21 zilizopendekezwa awali.
“Waliokuwa katika kamati, ni Godwin Nyelo (Madini), John Mpembelwa (BoT), Justo Tongola (BoT), Malemo Abella (BoT mshauri wa Gavana) na Mbatia (BoT),” alidai Mbatia.
Alidai kamati hiyo, watano walifanya kazi ya kutafuta kampuni, walipata kampuni 21 na baada ya kufanya upembuzi walibakia na kampuni tano, walipotakiwa kuwasilisha nyaraka mbalimbali, kampuni mbili zilifanikiwa kujibu.
“Kampuni moja ilikubali kufanya kazi kwa malipo ya asilimia 2 ya kazi nzima na Kampuni ya Alex Stewart ilikubali kufanya kazi kwa malipo ya asilimia 1.9 ya kazi yote nje ya kodi za Tanzania na kwamba kama zingekuwepo asingehusika nazo,” alidai.
Mbatia alidai baada ya kukubalika Kampuni ya M/S Alex Stewart, walipeleka mapendekezo kwa Gavana ambaye alichukua jukumu la kumwalika mwakilishi kutoka katika kampuni hiyo kwa ajili ya kufanya mjadala wa makubaliano.
Shahidi huyo wa utetezi alidai walipokubaliana BoT iliipa kampuni hiyo mkataba wa miaka miwili uliosainiwa kati ya mwakilishi wa kampuni na BoT, ulipomalizika Gavana aliwaongeza mkataba mwingine wa miaka miwili.
Mbali na Mramba, wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Daniel Yona na Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Fedha, Gray Mgonja,
Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali harasa ya Sh bilioni 11.7 kwa kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya M/S Alex Stewart ya nchini Uingereza, ambapo wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Agosti 2002 na Juni 2004, Dar es Salaam.

Post a Comment