Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

ZANZIBAR YAAZIMISHA SIKU YA AFYA KWA MTOTO

 

   
 
01
Docta Yasin Hamza akimfanyia uchunguzi wa meno mmoja kati ya wanafunzi wa Skuli za Maandalizi katika maadhimisho ya Afya ya mtoto yaliyofanyika  Kijiji cha Chwaka.02Wanafunzi wa Skuli za Maandalizi Chwaka na Jendele wakionyesha michezo katika maadhimisho ya siku ya Afya ya Mtoto03
Mgeni Rasmin wa maadhimi ya siku ya Afya ya mtoto Mussa  Mwadini Mcha akizungumza na Wazazi na Walezi wa skuli za Maandalizi. kuliani kwake Mratibu wa Jumuiya ya Skuli za Maandalizi za Madrasa Mohamed Othman na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Skuli ya Maandalizi ya Madrasati Maamur ya Chwaka.

Picha na Ramadhan Ali wa Maelezo Zanzibar.
Na Ali Issa na Miza Othman Maelezo-Zanzibar             
Wazazi na Walezi wa vijiji vya Chwaka na vijiji vya jirani wameshauriwa  kuwapeleka watoto wao Skuli za Maandalizi mapema wakiwa na umri wa miaka mitatu  ili kuwajengea uwezo wa ufahamu wakiwa bado wadogo.
Hayo yameelezwa leo na Katibu wa Kamati ya Maendeo ya kijiji hicho  Mussa Mwadini Mcha wakati alipokuwa akizungumza na wazazi na wanafunzi wa skuli za maandalizi  za vijiji vya Chwaka na Jendele katika Madhimisho ya siku ya Afya ya Mtoto zilizoandaliwa na Zanzibar                    Madrasa Resouce Centre  (ZMRC) zilizofanyika kijijini hapo.
Amesema kumpeleka mototo skuli katika umri huo ni  kumkuza kiakili na kimwili na hatimae katika umri  wa utuuzima mtoto huyo huwa na ufahamu mkubwa.
“Nivizuri kumpeleka skuli mtoto akiwa na umri wa chini ya mika minne kwani kufanya hivyo inampelekea  mototo kuwa na akili nzuri na kumuandaa mapema na elimu ya msingi,” alisema Mussa Mwadini.
Aidha aliwafahamisha wazee  hao kuwapatia watoto chakula  mchanganyiko chenye kujenga mwili ili  wawe na Afya na ukuaji na kukua vizuri.
Nao walimu wa Madrsa hizo walielezea changamoto zinazo wakabilikatika skuli zao ikiwemo uhaba wa vikalio, vifaa vya kusomea na kukosa uzio katika skuli zao ambapo baadhi ya watu huingia na  waharibifu na kuharibu mazingira ya skuli zao.
“Uzio ni tatizo kubwa katika skuli zetu za maandalizi na mara nyingi tunashindwa kuweka pembea za kuchezea kwa kuhofia kuharibiwa na watu wasiopenda maendeleo yetu”,alisema Batuli Abdi  Mwalimu wa  Skuli ya Jendele.
Hata hivyo walimu hao wamelalamikia  ushirikiano mdogo kati yao na  wazazi wa wanafunzi  wakati wanapoitwa katika Madrasa hizo jambo ambalo linarudisha myuma maendelea kwa walimu na wanafunzi wao.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top