Meneja
Uhusiano na Mawasiliano wa Shirika la Taifa la Maendeleo(NDC) Abel
Ngapemba(kushoto) akieleza kwa waandishi wa habari juu ya mpango wa
Serikali kuzalisha tani milioni moja kwa mwaka mara uzalishaji wa
madini ya chuma utakapoanza mwaka 2018/19 chini ya kampuni ya Tanzania
China Mineral Resources Limited (TCIMRL) na kuwa moja ya wazalishaji
wakubwa wa madini hayo barani Afrika, wakati wa mkutano uliofanyika
ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO),kulia ni Afisa Habari wa Idara ya
Habari Bi.Fatma Salum.
Mkuu
wa Kitengo cha Viwanda vya Kemikali toka Shirika la Taifa la
Maendeleo(NDC) Abdallah Mandwanga akifafanua jambo kwa waandishi wa
habari kuhusu faida za uzalishaji wa madini ya Titanium takribani tani
175,400 na Vanadium tani 5,000 kwa mwaka, wakati wa mkutano uliofanyika
ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO).
Meneja
Uhusiano na Mawasiliano wa Shirika la Taifa la Maendeleo(NDC) Abel
Ngapemba(kushoto) akiwaonesha waandishi wa habari picha ya mchoro wa
kiwanda cha chuma cha liganga, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa
Idara ya Habari(MAELEZO),kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari
Bi.Fatma Salum.
PICHA NA HASSAN SILAYO (MAELEZO)
Post a Comment