Msafara
wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
ukielekea Kata ya Dutwa Wilayani Bariadi Mkoa mpya wa Simiyu ambako
ametembelea mashina na miradi kadhaa ikiwa ni pamoja na kuhimiza
utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama hicho, Katibu Mkuu Kinana
ameongozana na Katibu wa Itikadi , Siasa na Uenezi wa CCM Ndugu Nape
Nnauye pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Simiyu na wilaya ya
Bariadi akiwemo Mbunge wa jimbo la Bariadi Magharibi Mh Andrew Chenge,
Katibu Mkuu huyo anamalizia ziara yake katika mkoa wa Simiyu kesho kwa
kufanya ziara katika jimbo la Busega na keshokutwa ataanza ziara katika
mkoa wa Mara akianzia Wilaya ya Bunda, Katika mkutano wa hadhara
uliofanyika leo kwenye soko la Dutwa Abdulrahman Kinana amesema Chama
cha Mapinduzi hakitakubali kuburuzwa na wapinzani ila kiko tayari
kukosolewa kwa hoja na si kwa matusi, kejeli na vitisho vya wanasiasa. Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa pili kutoka kulia ni Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Simiyu Mh. Dk Titus Kamani wakishirikiana na wananchi
kusogeza matofari katika eneo itakapojengwa nyumba ya mwenyekiti wa
shina namba 12 Isenge kijiji cha Igaganulwa Kata ya Dutwa ambapo Katibu
Mkuu huyo amfanya harambee na kukusanya michango mbalimbali kwa ajili
ya kununulia vifaa vya ujenzi wa nyumba hiyo. Mbunge
wa Jimbo la Bariadi Magharibi Mh. Andrew Chenge wa nne kutoka kulia ni
Pascal Mabiti Mkuu wa mkoa wa Simiyu wa tano wakishiriki katika zoezi la
kubeba matofali kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hiyo ya mwenyekiti wa
shina. Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kulia na Nape Nnauye Katibu wa NEC
Itikadi, Siasa na Uenezi wakishiriki kuchimba msingi kwa ajili ya
ujenzi wa nyumba hiyo inayojengwa katika kitongoji cha Isenge kata ya
Dutwa. Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Nape Nnauye akiwa amekaa pamoja na wananchi katika mkutano wa shina namba 12 Isenge kata ya Dutwa. Wananchama wa CCM shina la Isenge wakimsikiliza Katibu Mkuu hayupo pichani. Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kulia akishiriki kula chakula cha
kiasili cha kisukuma kinachoitwa Michembe, kutoka kushoto ni Mh. Andrew
Chenge Mbunge wa jimbo la Bariadi Magharibi, Pascala Mabiti Mkuu wa mkoa
wa Simiyuna Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Dk. Titus Kamani
wakishiriki kula chakula hicho. Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Nape Nnauye akila wali pamoja na wananchi katika kata hiyo Wakina
mama wakiendelea na biashara zao katika soko la Kata ya Dutwa ambalo
limejengwa na Serikali kwa kushirikiana na wananchi pamoja na mbunge wa
jimbo hilo. Biashara zikiendelea sokoni hapo. Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kulia kushoto akiongozana na
Mbunge wa jimbo la Bariadi Magharibi Mh. Andrew Chenge wakati akikagua
soko hilo. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiulizia bei ya Dagaa kwa Zawadi Malina Mchuuzi wa Dagaa katika soko hilo. Daud Njalu Silanga Mwenyekiti
wa UVCCM Mkoa wa Simiyuakinunua Kabichi kutoka kwa Marietha Maiko
mchuuzi wa mbogamboga katika soko hilo lililopo kata ya Dutwa Bariadi. Wananchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani wakati akizungumza katika soko la Dutwa. Mh. Andrew Chenge Mbunge wa jimbo la Bariadi Magharibi akizungumza na wananchi katika soko hilo. Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani akipokelewa na
wananchi kwa kunyanyua bendera juu ikiwa ni ishara ya ukaribisho rasmi
kwa Katibu Mkuu huyo. Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kujenga ukuta wa choo
cha shule katika shule ya sekondari ya Malambo katika halmashauri ya mji
ya Bariadi.(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-BARIADI SIMIYU)
Loading...
BLOG RAFIKI
-
-
Burhan awekewa vikwazo na Marekani12 hours ago
-
-
-
-
RUZUKU YA NISHATI SAFI KUWANUFAISHA WANANCHI20 hours ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
Post a Comment