“PRESS RELEASE” TAREHE 18. 09. 2013.
WILAYA YA MBEYA MJINI - AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA
KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO
TAREHE 17.09.2013 MAJIRA YA SAA 06:30HRS HUKO MWANJELWA BARABARA YA
MBEYA/IRINGA JIJI NA MKOA WA MBEYA. GARI T.387 BMN AINA YA TOYOTA
COASTER LIKIENDESHWA NA DEREVA HANSI S/O HUMPHREY, MIAKA 37, KYUSA,
MKAZI WA KYELA LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU WESTON S/O HEPA MWALINGO,
MIAKA 83, MSAFWA, MKAZI WA AIRPORT NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO
HAPO. CHANZO KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI
YA RUFAA MBEYA. DEREVA AMEKAMATWA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE
MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI
DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI
WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA
BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI - AJALI YA MPANDA PIKIPIKI KUMGONA MTEMBEA KWA
MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO
TAREHE 17.09.2013 MAJIRA YA SAA 18:30HRS HUKO MBALIZI BARABARA YA
TUNDUMA /MBEYA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA. PIKIPIKI NA
DEREVA ASIYEFAHAMIKA ILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU REUBEN S/O MWAKALOBO,
MIAKA 22, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA MBALIZI NA KUSABABISHA KIFO CHAKE
PAPO HAPO. CHANZO NI MWENDO KASI . MTUHUMIWA ALIKIMBIA NA PIKIPIKI MARA
BAADA YA TUKIO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI TEULE YA
IFISI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI
DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI
WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA
BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI
KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA NA PIKIPIKI
AZITOE ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO
AJISALIMISHE MWENYEWE MARA MOJA.
WILAYA YA KYELA – KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO
TAREHE 17.09.2013 MAJIRA YA SAA 20:00HRS HUKO KATIKA ENEO KYELA KATI
WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA
LUGANO S/O RICHARD, MIAKA 23, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA KYELA – KATI
AKIWA NA BHANGI GRAM 20. MBINU NI KUFICHA BHANGI HIYO KWENYE MFUKO WA
SURUALI YAKE. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI
ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME
CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
WILAYA YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA NOTI BANDIA.
MNAMO
TAREHE 17.09.2013 MAJIRA YA SAA 10:00HRS HUKO KATIKA BAR IITWAYO NURU
INN ENEO LA MBALIZI WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA. ALIKAMATWA
ERICK S/O JAMSON, MIAKA 25, MSAFWA, MKAZI WA NZOVWE AKIWA NA NOTI BANDIA
MOJA YA TSHS 10,000/= YENYE NAMBA – DT 2937833. MBINU NI KUTAKA KUNUNUA
VINYWAJI KWA KUTUMIA PESA HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE
MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA
POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII HASA KATIKA MAENEO YA
KIBIASHARA KUWA MAKINI NA MATUMIZI YA PESA ILI KUJIEPUSHA NA WATU
WANAOTUMIA PESA BANDIA . AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU
YA MTANDAO WA WATU WANAOMILIKI PESA BANDIA AZITOE KATIKA MAMLAKA
HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE.
Signed by:
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment