Mwandishi Jamal Osman amefanya mahojiano exclusive na msemaji wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab kuhusiana na sababu za kuishambulia mall ya Westgate.
Hii ni tafsiri ya Kiswahili ya mahojiano hayo yaliyofanywa kwa Kiingereza kwenye mtandao wa Channel4
Msemaji wa Al-Shabaab: Sababu ya kufanya
shambulio ni kuwalinda watu wetu na nchi yetu sababu Kenya ilitushambulia, bado
wanaendelea kushikilia sehemu ya ardhi yetu. Tumekuwa majirani wenye amani,
lakini wao ndio walitushambulia na tunajilinda.
Haijalishi kama wewe ni Muislamu ama Mkristo, sheria
inasema unatakiwa kujilinda mwenyewe dhidi ya yule
aliyekushambulia.
JO: Mmeua watu wa mataifa mengi wakiwemo
Waingereza, hamuogopi mataifa makubwa yatawatafuta?
Msemaji wa Al-Shabaab: Tumewaambia Wakenya na
wale wanaoenda Kenya kwamba hatuwezi kuvumilia kile Kenya inatufanyia.
Tuliwaambia tutajilinda wenyewe na tuliwaonya kuhusu kwenda
Kenya.
Wakenya wana damu yetu mikononi mwao. Mtu yeyote
aliyejiandaa kwenda Kenya lazima ajiandae na kukabiliana na ukweli huo, na
hatuwaogopi watu wa Ulaya ama Wamarekani sababu sisi si
wadhaifu.
Na tunasema hili kwa watu wa Ulaya na Wamarekani ambao
wamekuwa wakiwasaidia wale wanaotushambulia, muwaambie Wakenya waache uonevu wao
kama mnataka kuwa salama.
JO: Kwanini mliilenga mall ya
Westgate?
Msemaji wa Al-Shabaab: Sababu ya kwanini
tuliilenga mall ya Westgate, ni kwakuwa Wakenya na serikali yao wametumia
majeshi dhidi yetu, ni maadui wetu. Wamewatuma watu wao Somalia, wameiunga mkono
serikali yao kuishambulia nchi yetu. Kwetu, popote pale Kenya ni sawa,
tutawapiga popote tuwezapo.
Sababu tulilenga Westgate ni kwamba tunajua ni sehemu
ambayo wanajisikia maumivu zaidi. Ni kwasababu inaingiza hela nyingi na ipo
katikati ya jiji.
Ni sehemu wanasikia maumivu na kwasababu tulitaka
kutuma ujumbe na hatukutaka kuupoteza ujumbe wetu. Tulitaka ujumbe wetu umfikia
kile Mkenya.
JO: Wapiganaji wenu ndani ya mall bado
wanapigana?
Msemaji: Ni zaidi ya saa 27 sasa, wapo ndani na bado wameshika hatamu.
Msemaji: Ni zaidi ya saa 27 sasa, wapo ndani na bado wameshika hatamu.
JO: Nasikia kuna mpiganaji mwanamke ndani
pia?
Msemaji: Hatupeleki wanawake wetu kwenye uwanja
wa vita.
JO: Kitu gani mnategemea kitatokea sasa? Nini
litakuwa tokeo la hili?
Msemaji: Kama Mungu akipenda, tunategemea
Wakenya watapata ujumbe kwamba kama ukimwaga damu, damu yako itamwagika pia.
Kwao kujua kuwa hawawezi kushikilia Kismayu, Dhobley na Afmadow na wategemee
waishi kwa amani Nairobi. Huo ni ujumbe tunataka kuutuma
kwao.
JO. Kwenye jumbe zenu kupitia Twitter mnasema
huu ni mwanzo tu na mtaendelea, ama mmeshafikia malengo
yenu?
Msemaji: Tunasema kwa Kenya, iacheni nchi yetu.
Huo ni ujumbe wa kwanza. Na kama wakikataa kuiacha nchi yetu basi tutaanzisha
vita yenyewe.
JO: Hivyo matakwa yenu kwa Wakenya, ni kuiacha
nchi yenu kama wanataka amani?
Msemaji: Kama Wakenya wanataka amani, wanatakiwa kuiacha nchi yetu.
Msemaji: Kama Wakenya wanataka amani, wanatakiwa kuiacha nchi yetu.
JO: Kwanini mnawalenga watu wasio na
hatia?
Msemaji: Raia wa kigeni, wanatakiwa kuondoka
kwenye nchi hiyo (Kenya) kwasababu Wakenya na Al-Shabaab wapo kwenye mgogoro na
tunamwambia kila mtu – Kenya ni eneo la vita.
JO: Kwakuwa unasema raia wa kigeni na Waingereza
wana maslahi makubwa nchini Kenya, mna ujumbe gani
kwao?
Msemaji: Tunasema kwa Waingereza, kwakuwa tunaamini wanawasaidia Wakenyan na Wakenya ni watumwa wao, wao (Waingereza) wanatakiwa kuwaambia Wakenya, walitoe jeshi lao Somalia.
Na Waingereza wanajua Wasomali hawataka tamaa. Tuliwakatalia Waingereza mwanzoni, ambao wana nguvu kuliko Wakenya
Post a Comment