Picha mchoro wa kiwanda Mchuchuma
Core inspection
Drilling Rig servicing
SHIRIKA LA TAIFA LA MAENDELEO
Development House, Kivukoni Front/Ohio Street. S.L.P 2669, Dar es Salaam. TANZANIA
Simu: +255-22-2111460-4, Nukushi: +255-22 2113618. E-mail ndc@ndc.go.tz. Web:http://www.ndc.go.tz
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
DAR ES SALAAM: Tanzania
inatarajia kuwa mmoja wa wazalishaji wakubwa wa chuma barani Afrika kwa
kuzalisha tani milioni moja kwa mwaka mara uzalishaji wa madini hayo
utakapoanza mwaka 2018/19 chini ya kampuni ya Tanzania China Mineral
Resources Limited (TCIMRL), ambayo ni kampuni ya ubia kati ya Shirika la
Taifa la Maendeleo (NDC) na Shirika la Sichuan Hongda Group (SHG) ya
China.
Ripoti
ya utafiti wa TCIMRL ambayo ni sehemu ya maandalizi ya kuanzishwa mgodi
na kiwanda cha chuma katika eneo la Liganga wilayani Ludewa,
iliyofanywa katika eneo la kilomita za mraba 10 pekee inabainisha kuwapo
kwa tani milioni 219 za chuma ambazo zitadumu kwa zaidi ya miaka 70 kwa
uchimbaji wa juu (open cast mining). Eneo lililobakia lina kilomita za
mraba 156 na kukadiriwa kuwa na rasilimali kubwa zaidi.
Tanzania
itashika nafasi ya nne ikizifuatia nchi za Afrika Kusini itakayozalisha
bidhaa za chuma tani milioni 8.5 kwa mwaka, Misri tani milioni 8.0 na
Libya tani milioni 2.0 kwa mwaka. Chuma kinachozalishwa duniani ni
takribani tani bilioni 1.55 kwa mwaka, mzalishaji mkubwa ikiwa ni China
inayotoa tani milioni 711 kwa mwaka ambayo ni sawa na asilimia 46 ya
chuma chote kinachozalishwa duniani.
Mbali na chuma, madini mengine yatakayotokana na mgodi huo ni Titanium tani 175,400 kwa mwaka na Vanadium tani 5,000 kwa mwaka.
Mradi
huu ni moja ya miradi miwili iliyopo katika mkataba kati ya NDC na SHG
uliotiwa saini Septemba 21, 2011 ya uanzishwaji wa mgodi wa makaa ya
mawe na ujenzi wa kituo cha kufua umeme wa megawati 600 katika eneo la
Mchuchuma pamoja na ujenzi wa msongo wa umeme wa kilovoti 220 kati ya
Mchumchuma na Liganga; na uanzishwaji wa mgodi wa chuma na ujenzi wa
kiwanda cha kuchenjua chuma na kiwanda cha kuzalisha bidhaa za chuma,
pamoja na ujenzi wa barabara kati ya Mchuchuma na Liganga.
Kiasi
cha Makaa ya mawe kulingana na utafiti wa TCIMRL katika eneo la
kilomita za mraba 30 ni tani milioni 370 ambazo zinaweza kuchimbwa kwa
miaka zaidi ya 100. Kkuna eneo la ziada la kilomita za mraba 110 ambalo
linakadiriwa kuwa na rasilimali zaidi ya makaa yam awe.
Miradi
hii miwili itakayogharimu Dola za Kimarekani bilioni tatu (USD 3.0bil)
inatarajiwa kuliingizia taifa mapato ya Dola bilioni 1.7 kwa mwaka
itakapoanza uzalishaji kamili mwaka 2018/19, mapato ambayo yatatokana na
uuzaji wa umeme wa megawati 600, uuzaji wa makaa ya mawe kwa nishati ya
viwandani, chuma, titanium, vanadium na itatoa ajira ya moja kwa moja
watanzania 6,000 na 35,000 kwa zisizo za moja kwa moja.
Miradi
hii hivi sasa ipo katika awamu ya kwanza ambayo ilikuwa inahusisha
utafiti na maandalizi kabla ya Mei mwakani kuingia katika awamu ya
ujenzi wa migodi na viwanda katika maeneo ya Mchuchuma na Liganga.
Mradi
huu wa ubia na mwekezaji wa kimataifa unakwenda sambamba na mradi
mwingine katika eneo hilo la Ludewa uliotiwa saini Septemba 2, 2009 na
kampuni ya wazawa ya M.M. Steel Resources Public Limited Company (MMSR
PLC). Mradi huu unalenga kuzalisha chuma ghafi kwa kutumia chuma cha
Liganga Matitu na makaa ya mawe ya Katewaka. Kampuni ya ubia
iliyoanzishwa ni Maganga Matitu Resource Development Limited (MMRDL).
Uwekezaji utakuwa ni dola za Kimarekani milioni 150 na unatazamiwa
kuingiza mapato ya dola milioni 183.3 kwa mwaka. Chuma ghafi hiki
kitatumika kuwa malighafi kwa viwanda vingine vilivyo ndani na nje ya
nchi, hivyo kuwezesha uzalishaji wa chuma imara kulikoni hiki cha sasa
kitokanacho na scrap ambacho ni hafifu. Lakini pia hujuma kwa
miundombinu yetu kwa ajili ya scrap utakoma.
Imetolewa na: Abel Ngapemba
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Shirika
angapemba@ndc.go.tz, 022 211 1490 0784 273 588/0715
18 Septemba 2013
Post a Comment