Jengo la RITA linalojengwa.
WAFANYAKAZI wa kampuni ya ujenzi ya China
Railway Jianchang Engineering Co. (T) Ltd - (CRJ) iliyochukua tenda ya
kujenga ghorofa la RITA maarufu kama RITA TOWER jijini Dar, wameingia
katika mgomo kwa kile kilichobainika kuwa wanadai malipo ya takribani
wiki mbili nzima.
Tukio hilo limetokea leo asubuhi maeneo ya Posta jijini Dar, ambapo wafanyakazi hao wamelalamikia malipo madogo kwa vibarua, masaa mengi ya kazi, malimbikizo ya malipo hayo pamoja na ulipaji wa njia ya mtandao ambao wameupinga kuwa umekuwa wa kinyonyaji kwa kuwa njia hiyo ni rahisi kuwaibia kwa kuwa hawasaini.
Akiongea kwa jazba Meneja wa saiti hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Mr. Dave, alisema kuwa kampuni yake haina matatizo katika ulipaji wa mishahara, lakini tatizo lipo kwenye mtandao wa simu ambao unashughulikia ulipaji wa fedha kwa wafanyakazi.
Meneja huyo aliahidi kuwa asubuhi ya leo haitapita bila kulipa pesa za wafanyakazi hao, ambao walionekana kushikilia msimamo wao japo kuwa waliombwa kuendelea na kazi.
Hadi kamera yetu inaondoka eneo la tukio hakukuwa na malipo yoyote yaliyofanyika na mgomo ulikuwa ukiendelea.

(Picha: Chande Abdallah / GPL)
Post a Comment