WATU nane wamefariki
katika matukio matatu ya usalama barabarani mkoani Mbeya.
Kwa mujibu wa taarifa
ya kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Diwani Athumani, imesema kuwa MNAMO TAREHE 22.09.2013 MAJIRA YA SAA 20:00HRS HUKO SOKOMATOLA BARABARA YA
SOKOMATOLA/STENDI KUU JIJI NA MKOA
WA MBEYA.
GARI T.223 AGQ AINA YA TOYOTA HIACE LIKIENDESHWA NA DUNIA S/O FRANSIS, MIAKA 38, MNGONI, MKAZI WA AIR PORT LILIACHA
NJIA KISHA KUPINDUKA NA KUSABABISHA VIFO
VYA ABIRIA SITA, KATI YAO WANAUME WANNE NA WANAWAKE WAWILI
AMBAO BADO HAWAJAFAHAMIKA MAJINA WALA ANUANI ZAO.
AIDHA
KATIKA AJALI HIYO WATU SABA
WALIJERUHIWA AMBAO NI 1. JUMA S/O WARIOBA, MIAKA 32, MKAZI WA
SAE 2. MWANDELA S/O MWAMSI, MIAKA
22, MKAZI WA MAJENGO 3. KAMBI S/O ALLY,
MIAKA 32, MKAZI WA IRINGA 4. SELEMAN S/O
SHELUKINDO, MIAKA 25, MSAMBAA, MKAZI WA ILEJE 5.NURU S/O SHELUKINDO, MIAKA 32, MSAMBAA, MKAZI WA ILEJE 6. BAHATI D/O ALLY, MIAKA 14, MKAZI WA
SONGEA NA 7. DUNIA S/O FRANSIS AMBAO
WOTE WAMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
CHANZO KINAENDELEA
KUCHUNGUZWA JAPO TAARIFA ZA AWALI ZINAONYESHA KUWEPO KWA HITILAFU KWENYE BREAK.. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA
RUFAA MBEYA. DEREVA AMEKAMATWA, NA ANAENDELEA KUHOJIWA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI
WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI
KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA WANANCHI KUFIKA
HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA AJILI YA UTAMBUZI WA MIILI YA MAREHEMU.
WILAYA YA
RUNGWE – AJALI YA GARI KUMGONGA MWENDESHA PIKIPIKI NA
KUSABABISHA KIFO.
KUSABABISHA KIFO.
|
MNAMO TAREHE
22.09.2013 MAJIRA YA
SAA 19:00HRS HUKO SOGEA BARABARA YA MBEYA/TUKUYU
WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. GARI T.131 AVN AINA YA TOYOTA
ESCUDO LIKIENDESHWA NA DEREVA PETER S/O MWAIKEMA, MIAKA 20, KYUSA,
MKAZI WA KIWIRA LILIMGONGA MPANDA PIKIPIKI MTAFYA
S/O AFYUSISYE MTAFYA , MIAKA 39, KYUSA, MWALIMU WA RUNGWE S/MSINGI,MKAZI WA
TUKUYU ALIYEKUWA AKIENDESHA PIKIPIKI AMBAYO
HAIKUFAHAMIKA NAMBA ZA USAJILI WALA AINA YAKE
NA KUSABABISHA KIFO CHAKE WAKATI ANAPATIWA MATIBABU HOSPITALI YA MISHENI IGOGWE. CHANZO NI MWENDO KASI WA GARI.
DEREVA AMEKAMATWA TARATIBU ZINAFANYWA ILI
AFIKISHWE MAHAKAMANI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO.
WILAYA YA
MBEYA VIJIJINI - AJALI YA PIKIPIKI KUMGONGA MPANDA
BAISKELI NA KUSABABISHA KIFO.
BAISKELI NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 22.09.2013 MAJIRA YA SAA
17:50HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA IPENJA
KATA YA MAENDELEO – USOHA WILAYA
YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA.
PIKIPIKI T.559 CDC AINA YA T-BETTER IKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI ILIMGONGA MPANDA BAISKELI PIUS S/O MENGO, MIAKA 15,
MSAFWA, MKAZI WA IPENJA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO.
CHANZO
KINACHUNGUZWA.
DEREVA ALIKIMBIA NA KUITELEKEZA PIKIPIKI ENEO LA TUKIO. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA
JUU YA MAHALI ALIPO DEREVA ALIYEHUSIKA KATIKA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA
HUSIKA ILI AKAMATWE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MARA MOJA.
WILAYA YA
CHUNYA – KUPATIKANA NA SILAHA [GOBOLE] BILA KIBALI.
MNAMO TAREHE 22.09.2013 MAJIRA YA SAA
16:55HRS HUKO KATIKA HIFADHI YA TAIFA
YA PITI [PITI GAME RESERVE]
WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA.
ASKARI POLISI
WAKIWA DORIA KWA KUSHIRIKIANA NA ASKARI WA WANYAMA PORI WALIMKAMATA EMANUEL S/O HOLMAN, MIAKA
52,MNYAMWEZI,MKULIMA,MKAZI WA KIJIJI CHA KITIDA AKIWA NA SILAHA MOJA BUNDUKI
AINA YA GOBOLE KATIKA HIFADHI HIYO BILA KIBALI. MTUHUMIWA NI MUWINDAJI
HARAMU.
TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI
ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA
MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI
ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Post a Comment