Na Ray Said, Bumbuli
WAZIRI
wa Chakula, Kilimo na Ushirika, Injinia Christopher
Chizza, amependekeza kuundwa kwa menejimenti ya muda katika kiwanda cha chai
cha Mponde kama njia ya kusuluhisha mgogoro uliopo kati ya
wakulima wa chai na mwekezaji wa kiwanda hicho, Kampuni ya Chai
Lushoto.
Injinia Christopher
Chizza, katikati.
Akizungumza
katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika
uwanja wa mazoezi katika kata ya Mponde, Chiza pia aliahidi
kushughulikia mgogoro uliopo kati ya wakulima hao wa chai na mwekezaji wa
kiwanda cha chai cha Mponde, kilichopo Bumbuli, mkoani Tanga, ili kiendelee kutoa
huduma bora.
Alisema katika kumaliza mgogoro huo, atazungumza na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuhusu suala hilo ili kusaidia kupata ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro huo.
Alisema katika kumaliza mgogoro huo, atazungumza na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuhusu suala hilo ili kusaidia kupata ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro huo.
"Nitaishauri serikali kuchukua
kiwanda hicho na baadaye kuwakabidhi wananchi
ambao ndio wamiliki wa kiwanda hicho,"
alisema.
Mgogoro kati ya wakulima na mwekezaji unatokana na madai ya
wakulima hao kuelezea kuwapo kwa upotevu wa fedha kiwandani na viongozi wa
Chama cha Utega, hivyo kupoteza imani kwa wakulima kwa madai kuwa wapo upande
wa mwekezaji anayewanyonya wakulima wa chai.
Waziri huyo pia alisema watapeleka wakaguzi kutoka
serikalini kuchunguza kama kuna ubadhirifu wowote
kiwandani hapo ili kuwasaidia wakulima wa chai kupata haki yao
na kulisaidia zao hilo ambalo ndio kitega uchumi.
Waziri Chiza alisema kuwa ana
imani uchunguzi utakaofanywa na wakaguzi kutoka
serikalini utaleta majibu mazuri kwa kuwa utaonyesha
kuna ubadhirifu.
Alisema wao upande serikali hawawezi
kuendelea kuona zao la chai linaoza,
hivyo lazima lithaminishwe kwa kuuzwa kwenye viwanda
vingine na lazima mgogoro huo upatiwe ufumbuzi.
“Tutamaliza mgogoro huu kwa
kupata suluhisho la haraka ili wakulima
wapate haki yao ya msingi na badae
waendelee kulilinda zao la chai kama
ilivyokuwa zamani,” alisema Waziri huyo.
Waziri huyo alisema kuwa Chama cha UTEGA lazima kifanye mkutano mkuu ili kujadili matatizo yanayokikabili na akaahidi kuwa serikali iko tayari kutoa fedha kwa ajili ya kugharamia mkutano huo.
pia aliahidi kuwa Wizara yake na Wizara ya Viwanda na Biashara wa kushiriiana na Wizara ya Mambo ya Ndani watafanya ukaguzi wa Chama hicho ili kujua kama kinaendeshwa kwa mujibu wa kanuni na sheria za Tanzania.
Wakulima hao wakizungumza katika mkutano huo wa kujadili kero mbalimbali ambazo zinawakabili, walisema kuwa wako tayari kukosa fedha kwa kipindi chote ambacho kiwanda kitakuwa kimefungwa kuliko kuendelea kunyanyaswa na wawekezaji hao.

Post a Comment