Mgeni
rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akitoa
hotuba ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama
Barabarani iliyozinduliwa Kitaifa jijini Mwanza leo. Wa pili kulia ni
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza
Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo na kulia ni Kamanda wa Polisi Kikosi
cha Usalama Barabarani Tanzania, SACP Mohamed Mpinga. Kauli mbiu ya
Maadhimisho ya mwaka huu ni “USALAMA BARABARANI UNAANZA NA MIMI, WEWE NA
SISI SOTE”. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Polisi
kutoka Trafiki Makao Makuu jijini Dar es salaam, Dumu Mwalugenge,
akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk
Emmanuel Nchimbi (kushoto), namna ajali barabarani zinaweza kuepukika
endapo watumiaji barabara watakuwa waangalifu kwa kufuata sheria za
barabarani. Waziri Nchimbi aliyazindua maonesho hayo ya Wiki ya Nenda
kwa Usalama Barabarani katika Kiwanja cha Mpira CCM Kirumba jijini
Mwanza leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “USALAMA
BARABARANI UNAANZA NA MIMI, WEWE NA SISI SOTE”. Picha na Felix Mwagara,
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waendesha
pikipiki (bodaboda) na baiskeli nao pia walishiriki kikamilifu katika
uzinduzi wa maonesho hayo yaliyofanyika katika Kiwanja cha Mpira cha CCM
Kirumba, jijini Mwanza leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni
“USALAMA BARABARANI UNAANZA NA MIMI, WEWE NA SISI SOTE”Picha na Felix
Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (watano kutoka kushoto),
Naibu Waziri wa wizara hiyo na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama
Barabarani, Pereira Ame Silima (katikati) pamoja na maafisa usalama
barabarani na wadau wa usalama barabarani wakiwa katika picha ya pamoja
baada ya uzinduzi wa maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani
ambayo Kitaifa yamezinduliwa na Waziri Nchimbi, jijini Mwanza leo. Kauli
mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “USALAMA BARABARANI UNAANZA NA
MIMI, WEWE NA SISI SOTE”. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
Post a Comment