Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Papa John Paul kutangazwa mtakatifu Aprili mwakani

 


zzzzzzzzzzzzpope_25f2f.jpgPapa John Paul II na John XXIII wanatarajiwa kutangazwa watakatifu Aprili 27 mwakani, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkuu wa sasa wa kanisa Katoliki, Papa Francis.
Taarifa ya uamuzi huo imetolewa leo kwenye mkutano wa makadinali unaoendelea mjini Vatican, ikiwa ni hatua mihimu ya kuthibitisha tangazo lake la Julai mwaka huu kwamba atawapa heshima viongozi hao wawili wa juu wa Kanisa waliopita katika karne ya 20.
Katika taarifa iliyonakiliwa kutoka kwenye gazeti la mtandaoni la Daily Mail, alisema wakuu hao wa Kanisa Katoliki duniani ambao kwa sasa ni marehemu waliweza kutumia karama zao kwa uamunifu na kuonyesha matendo makuu.
Wachambuzi wa masuala ya Kanisa hilo alieleza kwamba inaonekana umuzi huo ni wa makusudi ikiwa ni hatua ya kujaribu kuliunganisha kanisa hilo ambalo lina mkanganyiko kwa sasa.
Kila mmoja ana watu wanaomuunga mkono na wanaompinga, ambapo kwa sasa Francis anaonekana kuungwa mkono na wote wa pande zote mbili hivyo kuwa kichocheo cha kuunganisha na kufuta makovu yaliyolikumba Kanisa hilo kwa miaka ya hivi karibuni.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top