Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili Uwanja wa Ndege wa Nduli mjini Iringa
leo Oktoba 13, 2013 kuhudhuria Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenye
wa Uhuru, Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere zitaziofabyika kesho (Oktoba 14, 2013) katika uwanja
wa Kumbukumbu ya Samora. PICHA NA IKULU.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na kamanda wa vijana Iringa Mhe Asas
katika Uwanja wa Ndege wa Nduli mjini Iringa leo Oktoba 13, 2013
kuhudhuria Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenye wa Uhuru, Wiki ya
Vijana na Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
zitaziofabyika kesho (Oktoba 14, 2013) katika uwanja wa Kumbukumbu ya
Samora
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Iringa mjini Mhe Msigwa
katika Uwanja wa Ndege wa Nduli mjini Iringa leo Oktoba 13, 2013
kuhudhuria Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenye wa Uhuru, Wiki ya
Vijana na Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
zitaziofabyika kesho (Oktoba 14, 2013) katika uwanja wa Kumbukumbu ya
Samora.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini Iringa jioni ya leo, Jumapili, Oktoba 13, 2013, kwa ziara ya siku mbili ya kikazi mkoani Iringa. Rais Kikwete amefuatana na Mama Salma Kikwete.
Shughuli kubwa ambazo Mheshimiwa Rais atazifanya wakati wa ziara hiyo ni kushiriki Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kuwa mgeni rasmi katika Kilele cha Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka huu wa 2013 na Kilele cha Wiki ya Vijana.
Ndege iliyombeba Rais Kikwete ilitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Nduli mjini Iringa kiasi cha saa 12.20 jioni na kulakiwa na umati mkubwa wa wananchi wakiwemo wafuasi wa vyama vya siasa vikiwamo CCM na Chadema.
Post a Comment