Rais
wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete (kushoto) na Rais wa Rwanda,
Mhe. Paul Kagame, nchi zao zimetajwa kuwa na utawala bora katika jumuiya
ya Afrika mashariki
……………………………………………………………………………………………………………………………
Mahmoud Ahmad Arusha
Tasisi ya Mo Ibrahim juu ya Utawala Bora Afrika, imebaini nchi za Rwanda na Tanzania kuwa nchi zenye utawala bora zaidi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kati ya nchi 52 za kiafrika.
Tasisi ya Mo Ibrahim juu ya Utawala Bora Afrika, imebaini nchi za Rwanda na Tanzania kuwa nchi zenye utawala bora zaidi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kati ya nchi 52 za kiafrika.
Kwa
mujibu wa ripoti iliyotolewa Jumatatu na taasisis ya Mo Ibrahim imesema
Rwanda imepata wastani wa asilimia 57.8 ikiwa ni zaidi ya wastani wa
kiafrika wa asilimia 51.6.
Hii
inamaanisha kwamba nchi hiyo imeboresha utawala bora kwa zaidi ya
asilimia 10.9 tangu mwaka 2000, ikiwa nafasi ya kwanza kwa nchi za
Afrika mashariki ikifuatiwa na Tanzania iliyoshika nafasi ya 17 barani
Afrika kwa kupata asilimia 56.9 huku Uganda ikiwa ya tatu ECA kwa kuwa
ya 18 kwa kupata asilimia 56. Kenya imekuwa ya 21 na kushika nafasi ya
nne kwa kupata asilimia 53.6 huku Burundi iliyopata asilimia 43.8
ikishika nafasi tano kwa EAC.
”Rwanda
imekuwa ikifanya vizuri mwaka hadi mwaka tangu mwaka 2000, ikiwa ni
maboresho makubwa zaidi katika nyanja ya Maendeleo ya Binadamu hususa ni
katika sekta ya elimu na afya,” ripote ilisema.
Mauritania
imeshika nafasi ya kwanza katika Afrika kwa kupata asilimia 82.9
ikifuatiwa na Botswana aliyopata asilimia 77.6 ambapo Cape Verde
imeshika nafasi ya tatu kwa kupata asilimia 76.7. barani.
Ripoti
hiyo imebaini kwamba asilimia 94 ya nchi za Afrika ikiwemo Rwanda watu
wake wanaishi katika nchi ambazo zimeboresha kwa ujumla masuala ya
utawala bora tangu mwaka 2000.
Asilimia
sita ya watu wanaoishi kwenye nchi ambazo kiwango cha utawala bora
kimeshuka tangu mwaka 2000 ni pamoja na nchi za Guinea-Bissau,
Madagascar, Somalia, Libya na Mali.
Taasisi hiyo ya Mo Ibrahim pia hutoa tuzo kwa viongozi bora barani Afrika.Hata hivyo tuzo hiyo haijatolewa kwa mara ya nne sasa.
Tuzo
hiyo hotolewa kwa kiongozi wa Afrika aliyechaguliwa kidemokrasia
aliyeonesha kwa vitendo uongozi bora,kutumikia muhula wake wa uongozi na
kuachia ngazi miaka mitatu iliyopita.
JT/LC/NI
Post a Comment