Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Simu ya mkononi yasababisha mkazi wa Sengerema kujilipua na moto

 

WADAU TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIYO HAPO CHINI KAMA ITAKUWA IMEKUKWAZA LAKINI NDIO HALI HALISI YA TUKIO LENYEWE.
ZACHARIA GINDU(ALIVYOJILIPUA) Na Daniel Makaka
Marehemu Zakaria Gindu baada ya kujilipua na moto.
 Na Daniel Makaka wa Mo Blog Sengerema,
 Mkazi wa kitongoji cha Kijiweni kilichopo kijiji cha Chifunfu kata ya Chifunfu wilaynia Sengerema mkoa Mwanza, amefariki dunia baada yakujilipua kwa moto kisha kuungua vibaya na kufariki dunia akiwa ndani ya nyumba yake.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mwenyekiti wa kitingoji hicho Bw. Juma Mashauri, amemtaja aliyekumbwa na mauti hayo kuwa ni Bw. Zakaria Ngindu (36) mzaliwa wa kijiji cha Mwamanyiri wilaya ya Busega  Mkoa wa Simiyu.
Bw. Mashauri amesema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo Septemba 27 mwaka huu majira ya saa10 jioni na chanzo cha tukio hilo inaelezwa kuwa ni kutokana na ugomvi uliokuwa ukiendelea ndani ya nyumba yake na mke wake alitajwa kwa jina la Veronica Lumanicha mzaliwa wa kitongoji cha NGOMA ‘B’ Kilichopo kijiji cha Nyamatongo Kata ya Nyamatongo wilayani Sengerema, baada ya kumkuta akiwa na namba za simu ya mkononi ambazo hazieleweki kuwa ni za nani.
ZACHARIA GINDU(Alivyojilipua) Na Daniel Makaka (2)
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo walisema wanandoa hao walikuwa na ugomvi wa mara kwa mara wakituhumiana kutokuaminiana katika ndoa yao iliyokuwa imegubikwa na vitimbwi vingi vililosababisha mmoja wa wa wanandoa hao kushikwa na hasira na kunywa pombe kisha kuchukuwa maamuzi ya kujiua ili kuondokana na kero hiyo.
Kutokana na tukio hilo kwa upande wake  Katibu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya Sengerema Bw.Benedictor Bujiku aliyekuwa ameambatana na waandishi wa habari kushuhudia tukio hilo amewaomba vijana kupenda kujishugulisha na shuguli na kuacha suala la ulevi unaopelekea kuchukua maamuzi ya kujiua angali taifa bado linawategemea .
Naye diwani wa kata hiyo ya Chifunfu Robert Madaha amesikitishwa kwa kutokea kwa tukio hilo na amewataka wananchi kuacha unywaji wa pombe ambao hauna faida yoyote kwa ujenzi wa Taifa.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top