Meneja Maboresho Swahili Fashion Week, Hamis K Omary akizungumzia uboreshwaji wa Swahili Fashion Week 2013.
Bw.
Honest Arroyal,Mratibu wa Mitindo Swahili Fashion Week (Kulia) na
Catherine Lumbanga, Mratibu wa Masoko Golden Tulip Hotel wakizungumzia
ujio mpya wa Swahili Fashion Week 2013.
Happy
Shame, (Kulia) Meneja Masoko wa EATV na Ea Radio akizungumzia mipango ya
EATV na Radio juu ya Swahili Fashion Week mwaka huu.
Mratibu
wa Masoko na Mauzo kutoka Hoteli ya Golden Tulip Bi. Catherine Lumbanga
akizungumzia jinsi hoteli yao inafurahi kushirikiana Swahili Fashion
Week kwa mwaka wa pili mfululizo.
Maonesho
ya sita ya Swahili Fashion Week yatafanyika Golden Tulip Hotel kuanzia
tarehe 5 mpaka 8 Desemba 2013, Dar Es Salaam, Tanzania.
Swahili
Fashion week 2013 itakusanya wabunifu 40 kutoka ndani na nje ya
Tanzania ili kuonesha mitindo yao, yenye kwenda na wakati na kutegemewa
kushika soko la Afrika Mashariki mwaka 2014.
“Swahili
Fashion Week mwaka huu ina lengo la kuifikia jamii zaidi, na kukuza
vipaji katika tasnia ya mitindo. Ni zaidi kuhusu kuthamini wabunifu wa
kwetu na kuwatengezea jina,huku tukiwapeleka ngazi za juu zaidi kila
mwaka” Akizungumza Bw. Washington Benbella, Meneja wa Swahili Fashion
Week
Ukiwa
ni mwaka wa 6 wa Swahili Fashion Week, Katika mashindano ya wabunifu
wanaochipukia, Waandaaji wamependekeza dhima ya mwaka huu (theme)
“Evolution” ambayo inawataka wabunifu chipukizi hao kubuni mavazi
yanayoashiria mabadiliko, si lazima upya, ila yenye muonekano wa
kitofauti na mzuri.
“Tunasisitiza
jamii iunge mkono tasnia ya mitindo na kuvaa mavazi ya kikwetu, hasa
kwa Tanzania. Vipaji vya nyumbani vinahitaji kukuzwa ili kufikia majina
yanayotambulika duniani katika tasnia hii. Hisani huanza nyumbani, na
ndio maana tunategemea kampuni pamoja na mashirika mbali mbali kusaidia
tasnia ya mitindo” Hamis K Omary, Meneja Masoko Swahili Fashion Week.
Swahili Fashion week imedhaminiwa na EATV, East Africa Radio, Golden Tulip Hotel, Eventlites, Push Mobile, BASATA (Baraza la Sanaa la Taifa), Ultimate Security, Global Outdoor Ltd na 361 Degrees.
Swahili Fashion week imedhaminiwa na EATV, East Africa Radio, Golden Tulip Hotel, Eventlites, Push Mobile, BASATA (Baraza la Sanaa la Taifa), Ultimate Security, Global Outdoor Ltd na 361 Degrees.
Swahili
Fashion Week is ni jukwaa la wabunifu wa mitindo na vito kutoka Nchi
zinazozungumza Kiswahili na Bara la Afrika kwa ujumla Kuonyesha ubunifu
wao, kutafuta masoko kwa ajili ya ubunifu na kujenga uhusiano na wateja
pamoja na tasnia ya mitindo kimataifa
Hii ni kwa nia ya kusisitiza kukua kwa mitindo katika kanda ya
Afrika Mashariki na Kati na njia ya kipato ihusishayo tasnia ya ubunifu, huku ikitangaza wazo la “Made in Africa”
Afrika Mashariki na Kati na njia ya kipato ihusishayo tasnia ya ubunifu, huku ikitangaza wazo la “Made in Africa”
Swahili
Fashion Week imeanzishwa na mbunifu mashuhuri Tanzania, Mustafa
Hassanali mwaka 2008. Mpaka sasa ndio maonyesho makubwa ya mitindo
katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati.
2013
Itakua ni maonyesho ya sita ya Swahili Fashion Week na Tuzo, ambayo
yatafanyika Dar es Salaam kuanzia tarehe 5 – 8 Desemba 2013.
Post a Comment