Meneja
wa Mradi wa Pamoja Tuwalee kutoka Taasisi ya Wanawake na
Maendeleo(WAMA) , Gloria Minja akizungumza jambo wakati wa majadiliano
ya kutengeneza ujumbe utakaohamasisha , Serikali , jamii na sekta
binafsi ili waweze kusaidia watoto waishio katika mazingira hatarishi
kuwapatia elimu , chakula na malazi leo jijini Dares Salaam.
Kaimu
Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) , Tabu
Likoko akifungua majadiliano ya kutengeneza ujumbe utakaohamasisha ,
Serikali , jamii na sekta binafsi ili waweze kusaidia watoto waishio
katika mazingira hatarishi kuwapatia elimu , chakula na malazi leo
jijini Dares Salaam.Kushoto ni mjumbe wa majadiliano hayo kutoka WAMA
,Julius Jacob
Mjumbe wa majadiliano ya kutengeneza ujumbe wa kuwatambua na kuwahudumia watoto waishio katika mazingira hatarishi , Asha Mtwangi akichambua ujumbe wenye kauli mbiu ‘ Pamoja Tuwalee’ inayosimamiwa na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) leo jijini Dares Salaam.
Mjumbe
wa majadiliano ya kutengeneza ujumbe wa kuwatambua na kuwahudumia
watoto waishio katika mazingira hatarishi, Peter Mabwe
akichambua ujumbe wenye kauli mbiu ‘ Pamoja Tuwalee’
inayosimamiwa na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo
(WAMA) leo jijini Dares Salaam.
|
Mjumbe wa majadiliano ya kutengeneza ujumbe wa kuwatambua na kuwahudumia watoto waishio katika mazingira hatarishi , Asha Mtwangi akichambua ujumbe wenye kauli mbiu ‘ Pamoja Tuwalee’ inayosimamiwa na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) leo jijini Dares Salaam.
Mtaalamu wa masuala ya ushauri
katika mitaala, uandishi na uhariri , Victor Msinde (katikati
)akichangia mada juu ya majadiliano ya kutengeneza ujumbe
utakaohamasisha , Serikali , jamii na sekta binafsi ili waweze kusaidia
watoto waishio katika mazingira hatarishi kuwapatia elimu , chakula na
malazi leo jijini Dares Salaam.Picha zote Eleuteri Mangi –MAELEZO.
---
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
SEKTA binafsi na taasisi
mbalimbali zimeshauriwa kufadhili katika kuwasaidia watoto wanaoshi
katika mazingira magumu badala ya kusaidaia matamasha pekee ikiwa ni
hatua mojawapo ya ya kuwapatia maisha bora , ikiwemo kupunguza
umasikini na tatizo hilo.
Kauli hiyo
imetolewa leo na Meneja wa Mradi wa Pamoja Tuwalee kutoka Taasisi ya
Wanawake na Maendeleo(WAMA) , Gloria Minja wakati wa majadiliano ya
kutengeneza ujumbe utakaohamasisha , Serikali , jamii na sekta binafsi
ili waweze kusaidia watoto hao.
“Tuzinaomba
sekta binafsi ikiwa ni moja wa wadau katika kusaidia watoto waishio
katika mazingira magumu katika malengo yao walijiwekea kupitia kipengele
cha Uwajibikaji katika jamii (yaani corporate social responsibilities)
kubadili mtanzamo wa kusaidia matamasha pekee ,bali waanze kufanya hivyo
kwa watoto hawa ili nao waweze kusoma ,kutibiwa na kupata malazi,”
alisema Gloria.
Alisema ikiwa
sekta hizo zitatekeleza wajibu huo,watoto hao wataweza kupata fursa ya
kusoma , kupata kazi na kuajiriwa katika maeneo mbalimbali ili waweze
kuendesha maisha yao.
Gloria
aliongeza kuwa mbali sekta hiyo , Serikali na kila mwanajamii
wanawajibu kutenga fedha kwa ajili ya kuwasaidia watoto hao , kwa
kufanya hivyo kutasaidia kuwawezesha kupata mahitaji muhimu na
kupunguza tatizo la umaskini nchini.
Akizungumzia
kuhusu ujumbe uliokuwa unatengenezwa na wadau hao kutoka sekta binafsi
na Serikali alisema lengo lake litakuwa ni kutoa ushawishi kwa jamii
nzima ili iweze kuwatambua na kuwahudumia watoto hao.
Aidha
alisema ujumbe huo utatumika kuhamasisha katika kampeni ya utetezi
kwa watoto hao ili Serikali, Jamii na sekta binafsi zitambue kuwa
jukumu la kuwalea watoto hao ni la pande zote.
Akifungua
majadiliano hayo Kaimu Katibu Mtendaji wa WAMA , Tabu Likoko alisema
kuwa taasisi hiyo inafanya kazi ya kusaidia elimu kwa watoto wa
kike, yatima na uwezeshaji kwa wanawake.
Mradi huo wa
Pamoja Tuwalee unatekelezwa katika mikoa ya Morogoro,Pwani, Dares
Salaam na Zanzibar kwa kipindi cha muda wa miaka mitatu,ambapo ulianza
kutekelezwa mwaka 2011 hadi mwaka 2013 na WAMA kwa ushirikiano wa
fhi360 chini ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani(USAID).
Post a Comment