wakishiriki maandamano ya kuadhimisha siku ya msichana Duniani
yaliyoandaliwa Jijini Tanga na Shirika la Tawode chini ya ufadhili wa
Ubalozi wa Denmark kupitia (DANIDA)
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na
Watoto,Ummy Mwalimu akiongoza maandamano ya wanawake walipokuwa
wakiingia uwanja wa Mkwakwani kusherehekea maadhimisho ya siku ya
msichana Duniani mbayo yalikwenda sambamba na uzinduzi wa mradi wa
kuwajengea uwezo wasichana wa mkoa wa Tanga unaoendeshwa na shirika la
Tawode chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Denmark kupitia (DANIDA)

………………………………………………………
Burhani Yakub,
Tanga.Serikali ya Denmark imeahidi kuendelea kutoa msaada kwa maeneo
mbalimbali nchini yatakayojikita katika kutoa kipaumbele cha elimu
kwa watoto wa kike ili kuwawezesha kuinua hali zao za maisha kiuchumi
na kiafya.

Ahadi hiyo ilitolewa na Mwakilishi wa balozi wa Denmark nchini,Ester
Msuya wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuwajengea uwezo wasichana wa
Mkoa wa Tanga unaoendeshwa na shirika la Tanga Woman Development
Initiative (Tawode)na kufadhiliwa na ubalozi huo kupitia DANIDA).

“Mkakati wa sasa wa Serikali ya Denmark kuhusu ushirikiano wa
maendeleo ya kimataifa unaitwa “Haki ya maisha bora”tunajua kwamba
uwekezaji ulio bora ambao Serikali yoyote inawaza kufanya ni
ku-elimisha watoto wa kike”alisema Msuya.

Mwakilishi huyo wa balozi alisema Serikali ya Denmark inaamini katika
haki za mtoto wa kike na mwanamke kupata elimu au angalau fursa ya
kupewa stadi za maisha ili kuishi maisha bora na kuchangia katika
maendeleo ya jamii kwa ujumla

Alilipongeza shirika la Tawode kwa kufanikisha mchakato wa kuanza kwa
mradi huo wa kuwajengea uwezo wasichana wa mkoa wa Tanga na akaahidi
kuwa ubalozi utatoa ushirikiano wa hali na mali ili kufanikisha mradi
huo.

Akitoa melezo kabla ya kuzinduliwa mradi huo,Mwenyekiti wa Tawode
ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto,Ummy
Mwalimu alisema lengo la kuendesha mradi huu ni kutokana na ukweli
kwamba mtoto wa akike anabiliwa na changamoto nyingi kuliko wa kiume
likiwamo suala la kutojitambua .

Alitolea mfano wa tafiti zilizopo za viashiria vya ukimwi na malaria
nchini zilizofanyika mwaka 2011 na 2012 zinaonyesha kiwango cha
maambukizi kwa wasichana ni cha juu kuliko wavulana hususani walio
katika umri wa miaka 23 na 24.

Alisema maambukizi kwa wasichana walio katika umri kwa kati ya miaka
23 na 24 ni asilimia 6.6 wkati kwa wavulana wa umri kama huo ni
asilimia 2.8 pekee.

Mradi huo ulizinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambaye alipokea
maandamano ya wanawake na wanafunzi wa kike kutoka shule mbalimbali
mkoani hapa na pia alikagua mabanda ya maonyesho ya kazi za mikono
zinazofanywa na wanawake.

Post a Comment