Mshtakiwa raia wa Ethiopia, Dekele Stephano
akiwa amelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro muda mfupi
baada ya kusomewa mashtaka na mahakama ya Morogoro mkoani Morogoro
kuftia kushindwa kusom
ewa mashtaka na wenzake kutokana na kuumwa. PICHA/JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
ewa mashtaka na wenzake kutokana na kuumwa. PICHA/JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
Raia wa Ethiopia 16 wakiwa katika mahakama ya hakimu mkazi Morogoro mara baada ya kusomewa mashtaka ya kuingia nchini bila kibali kufuatia kukamatwa kwa katika lori wakati wakisafirishwa kuelekea nchi jirani ya Mawila eneo Chamwino barabara kuu Iringa-Morogoro oktoba 12 mwaka huu mkoani Morogoro. PICHA/JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
Naibu Kamishna Uhamiaji na Mkuu wa kitengo cha Udhibiti wa Mipaka, Upelelezi na Mashtaka, Joseph Malumbu akizungumza na waandishi wa habari katika mahakama hiyo.
Mwendesha mashtaka wa idara ya Uhamiaji mkoa wa Morogoro, Hermana Foya akifafanua jambo kwa waandishi wa habri muda mfupi kabla ya kusomewa mashtka mmoja wa watuhuma hao katika hospitali ya mkoa wa Morogoro.
PICHA/JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
Na Juma Mtanda, Morogoro.
MAHAMAKA ya wilaya ya Morogoro imeahirisha kesi ya washtakiwa 16 ambao ni wahamiaji haramu raia wa Ethiopia ikisubiri upande wa mashtaka kupeleka mkalimani sambamba na kufunga dhamana kwa dereva wa gari iliyowasafirisha kufuatia mmoja wa wahamiaji hao kuwa mahututi katika hospitali ya Rufaa mkoani hapa.
Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo, Maua Yusufu alisema kuwa mahakama imezingatia ombi la upande wa mashtaka la kuahirisha kesi hiyo hadi hapo itakapokuja na mkalimani na kwamba washtakiwa hao walishindwa kujibu lolote licha ya kusomewa mashtaka yao kufuatia kutojua Kiswahili wala kiingereza.
Pia alisema kuwa mahakama hiyo imezingatia ombi la mwendesha mashtaka huyo la kuzuia dhamana kwa mshtakiwa namba 17 Ally Mhamango (45) mkazi wa chang’ombe DSM ambaye ni dereva wa gari lililowasafirisa wahamiaji hao kufuatia hali mbaya ya kiafya ya mshtakiwa namba 13 ambaye amelazwa katika hospitali ya rufaa mkoani hapa akiwa mahututi.
Awali mwendesha mashataka wa polisi Hermana Foya aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Sagai Dichamo, Dilamo Olele, Ailu Odilu, Taakali Telauti, Ikadu Atinato, Musa Godebo, Okine Haile, Asaba Wade, Elisido Alidodo, Dakiru Tabama, Charineti Adani, Tadala Tolole na Dekele Stephano ambaye yupo wodini mahututi. Aliwataja wengine kuwa ni Jamali Ekitu, Mamush Gabule, Dagafa Brano na Ally Mhamango, mtanzania na mkazi wa Jijiji Dar es Salaam.
Mwenedesha mashtaka huyo alidai mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao kwa pamoja huku wakijua kufanya hivyo ni kosa walikuwepo nchini kinyume cha sheria ya umahiaji ya mwaka 1995 iliyorekebishwa mwaka 2002 kwa kifungu namba 1 (i), na cha 2 kidogo cha sheria ya uhamiaji.
Alidai kuwa washtakiwa hao 16 ambao ni raia wa Ethiopia oktoba 12 mwaka huu, saa 8 usiku katika eneo la Chamwino kwenye barabara ya Morogoro inayokwenda Iringa walikutwa wakiwa nchini kinyume cha sheria za uhamiaji huku wakiwa hawana hati ya kusafiria.
Mwendesha mashtaka huyo alidai kuwa mshtakiwa namba 17 alikabiliwa na shtaka la kusaidia washtakiwa hao kuingia nchini bila kuwa na hati ya kusafiria sambamba na kuwaficha washtakiwa hao katika loli lenye namba za usajili T 707 CGY ambalo ni la mizigo na sio la kusafirishia abiria kinyume na sheria ya uhamiaji.
Hata hivyo dereva huyo alikana kuhusika na vitendo hivyo na hivyo kurudishwa rumande hadi kesi hiyo itakapotajwa tena oktoba 28 mwaka huu wakati mahakama iliyotembelea katika hospitali hiyo na kumsomea shtaka mhamiaji Dekele Stepheno ikisubiri hali ya mgonjwa huyo kuwa nzuri na upande wa mashtaka kupeleka mkalimani.
Post a Comment