Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WIZI MPYA WA MAGARI DAR WAIBUKA

 


06-aug-sukari1Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke Kanda Maalumu ya Da es Salaam, limamsaka tapeli mmoja wa magari madogo ambaye amekua akiwaibia watu mbalimbali kwa ulaghai.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Temeke, ACP Englibert Kiondo, amezitaja mbinu zinazotumiwa na tapeli huyo kuwa aamekuwa akipeleka gari bovu katika gereji Fulani na kuomba gari nyingine ya kutembelea hata kwa kukodisha wakati gari yake ikifanyiwa matengenezo.
Amesema aamara baada ya kupatiwa gari hiyo huondoka nayo moja kwa moja na kuitelekeza gari yake inayotengenezwa ambayo nayo kwa wakati huo inakuwa ni ya wizi.
Kamanda Kiondo amesema mara nyingi mtu anayetapeliwa hataweza kufahamu hadi pale gari aliyoiacha katika gereji husika kukamatwa na Polisi abaada ya kuibwa katikaa mazingira kama hayo katika maeneo mengine.

Amesema tapeli huyo anayejiita Juma Athumani ambaye pia anajifanya mfanyakazi wa Mamkala ya Bandari Jijini Dar es Salaam, kwa mara ya kwanza katika gereji moja iliyopo nyumba za Bandari Barabara ya Kilwa, alitelekeza gari ndogo aina ya Dihtsu yenye namba za usajili T. 856 BTM na kupatiwa gari nyingine yenye nambari T.209 ATP Toyota Corolla.
Kamanda Kiondo amesema wakati akiendelea kutafutwa kwa utapeli huo mtuhumiwa alikwenda katika gereji moja iliyopo eneo la Mwenge na kwenda kuitelekeza gari hiyo ambapo pia alichukua gari nyingine aina ya Toyota Sprinter kwa mtindo huo huo na kuondoka nayo.
Alisema ilipokamatwa aaaaagari hiyo mtuhumiwa huyo alikwenda akatika gereji moja iliyopo eneo la Ilala na kuitelekeza gari hiyo na kuchukua gari nyingine ndogo aina ya Vitz yenye namba za usajili T.946  BLW agari ambayo bado inatafutwa hadi sasa.
Amesema awali tapeli huyo alikuwa akitumia simu yenye nambari 0656 654167 iliyosajiliwa kwa jina la Juma Athuman lakini aabaadaye simu hiyo ikipigwaa inaonyesha kuwa imezimwa.
Kamanda Kioando ametoa wito kwa wananchi mbalimbali wakiwemo wamiliki wa magereji na maeneo ya kulaza magari Jijini kuwa macho na mtu huyo na kutoa taarifa Polisi akama watabaini gari iliyoegeshwa kwa muda mrefu katika maeneo yao ili lifanyiwe uchunguzi na kutoa wito pia kwa mtu mwenye vielelezo vya gari T.856 BTM aina ya Dihtsu kufika kituo cha Polisi barabara ya Kilwa kuitambua.
Naye mmoja ya watu waliotapeliwa magari yao kwa mtindo huo Jijini Dar es Salaam  Bw. John Isack, ameelezea jinsi alivyotapeliwa gari yake T.946 BLW Vitz rangi ya bluu na kusema kuwa siku ya tukio tapeli huyo alifika kwake eneo la Tabata Kimanga kutaka gari ya kukodi lakini baada ya kumwambia inauzwa aliichukua kwa kuijaribu na kumuachia gari nyingine ambayo kumbe ilikuwa ni ya wizi na kutoweka na gari hiyo hadi sasa.
Bw. John amesema baada ya kuona siku zimepita nyingi na alipokuwa akimpigia hapatikani aliamua kuipeleka gari hiyo kituo cha Polisi Pangani Ilala ambako Polisi walibaini kuwa kumbe gari hiyo pia ilikuwa ni ya wizi. Hata hivyo baadaye gari hiyo ilipata mwenyewe.
Hadi sasa Tapeli huyo amebainika kutapeli amagari manne na funguliwa kesi katika vituo vya Polisi Barabara ya Kilwa mkoa wa Temeke, Kijitonyama mkoa wa Kinondoni na Kituo cha Pangani mkoa wa Ilala vyote vya Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top