Mhe. NWMA, Dk. Binilith Mahenge akisikiliza maelezo akiwa juu ya tanki la kuhifadhi maji, mradi wa maji Ng’humbi.
Tenki la kuhifadhi maji, mradi wa maji Kibaigwa.
BRN yampeleka NWMA Dodoma
Mhe.
Naibu Waziri wa Maji, Dk. Binilith Mahenge ameendelea na ziara yake
mkoani Dodoma kuangalia utekelezaji wa miradi ya maji ya vijiji 10
katika Halmashauri za mkoa huo kupitia mpango wa Big Results Now.
“Serikali
ina dhamana ya kuhakikisha sekta ya maji inapiga hatua kubwa na kupitia
Wizara ya Maji, itahakikisha vijiji 10 katika Halmashauri zote nchini
zinapata maji kufikia Juni, 2015.” alisema Dk. Mahenge.
Dk.
Mahenge alisisitiza ni wakati wa viongozi kuanzia ngazi ya Halmashauri
kusimamia kwa ufanisi utekelezaji wa miradi hiyo kwa maendeleo ya nchi.
Kutokana na wananchi kutumia muda mwingi kutafuta maji baadala ya
kufanya shughuli za kila siku za maendeleo kama kilimo na elimu.
Aliagiza
ufuatiliaji na usimamizi wa karibu wa utekelezaji wa miradi
iliyopangwa, kwani bila hivyo hakutakuwa na mafanikio yoyote. Pia,
aliwaasa wananchi kushiriki katika kuchangia fedha kiasi kidogo kwa
ajili ya kuhakikisha miradi hiyo ili iwe endelevu na kudumu kwa vizazi
vijavyo.
Dk.
Mahenge alitembelea pia mradi wa Ntomoko, wilayani Kondoa kujionea
utekelezaji wake ambao umekua ukisuasua katika utekelezaji wake.
Ambapo
hakuridhishwa na utekelezaji wa mradi huo kwa ujumla, pamoja na kukuta
wingi wa maji katika mradi huo, huku miundombinu yake ikiwa hairidhishi.
Dk.
Mahenge aliagiza mapungufu yote ya mradi huo yafanyiwe kazi na
kuhakikisha unatekelezwa kwa haraka, kwani Waziri Mkuu alishatoa karibu
Sh. Bil 3 ili ukamilike, na unategemewa kumaliza tatizo la maji wilayani
Kondoa na maeneo jirani.
Vilevile,
Dk. Mahenge, alifanikiwa kutembelea miradi ya Chunyu, Kimagai, Kidenge,
Ng’humbi, Kibaigwa, na Mkoka kujionea maendeleo ya miradi hiyo hadi
kufikia sasa na kwa kiasi kikubwa alidhirishwa na hali aliyoiona katika
ziara yake hiyo.
Dk.
Mahenge yuko mjini Dodoma kwa ziara ya siku 5 kuhakikisha sekta na
ametembelea wilaya za Mpwapwa, Kongwa, Kondoa na Chemba na anategemea
kumaliza ziara yake leo Jumamosi.
Post a Comment