Mama
Salma Kikwete akipewa zawadi ya mkanda wa kimasai toka kwa mmoja wa
wazee wa kimasai ikiwa kama zawadi kwa Mheshimiwa Rais Kikwete.
Chifu wa Kimasai Tikwa Morezo (Oloiboni) akizungumza kwa niaba ya wazee wa Kimasai.
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia tukio hilo la warsha ya viongozi wa Kimila wa jamii ya wafugaji.
Mgeni Rasmi Mama Salma kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa.
.asilimia 40 ya watoto wa kike kukosa fursa ya elimu nchini
Na Damas Makangale, Moblog
Mama
Salma kikwete amesema kuwa elimu ni msingi utakaomwezesha kijana
kujiepusha na changamoto za aina mbalimbali kama mimba za utotoni,
maambukizi ya VVU na dawa za kulevya.
Akizungumza
kwenye uzinduzi wa warsha ya viongozi wa Kimila wa jamii ya wafugaji
jijini Dar es Salaam, Mama Kikwete amesema elimu inamuwezesha kijana
kutumia fursa za maendeleo ya kiuchumi zilizopo hapa nchini.
“kwa
bahati mbaya sana kutokana na sababu mbalimbali wasichana wameachwa
nyuma sana katika fursa za elimu kuanzia elimu ya sekondari hadi vyuo
vikuu,,” amesema
Mama
Kikwete alifafanua kwamba kwa kiasi kikubwa katika maeneo ya vijijini
ambapo asilimia 40 ya watoto wa kike wanakosa fursa ya kupata elimu
ukilinganisha na asilimia 29 ya watoto wa kiume waliokosa fursa ya
elimu.
Amesema
wasichana zaidi ya 55,000 wamekuwa wakifukuzwa shule kwa sababu
mbalimbali ikiwemo ya ujauzito katika kipindi cha muongo mmoja uliopita.


Post a Comment