Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwana wa Malkia Elizabeth II wa
Uingereza, Prince Charles, jijini Colombo, Sri Lanka, leo Novemba 15,
2013 pembeni ya mkutano wa Wakuu wa nchi za Junuiya ya Madola (CHOGM
2013) ambako Prince Charles, maarufu zaidi kama His Royal Highness the
Prince of Wales, anamwakilisha mama yake mwenye umri wa miaka 87 ambaye
hakuhudhuria kwa mara ya kwanza katika miaka 40 ya historia ya mkutano
huo unaofanyika kila baada ya miaka miwili katika nchi itayoteuliwa
mwishoni mwa mkutano. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe
Peter Kallaghe.
Malkia
Elizabeth wa II alihudhuria CHOGM kwa mara ya kwanza mwaka 1973 jijini
Ottawa, akiwa kakosa kikao cha mwaka 1971, na tokea hapo hajakosekana
tena hadi safari hii. Alikuwepo pia katika mkutano wa mwisho uliofanyika
mwaka 2011 jijini Perth,
Australia. Na hii ni mara ya kwanza kwa Prince Charles kumwakilisha
mama yake ambaye imesemekana hakwenda Sri Lanka kutokana na ushauri wa
kutosafiri umbali mrefu. Ila katika CHOGM 2007 iliyofanyika Kampala,
Uganda, yeye na mama yake walihudhuria pamoja.
Post a Comment