*******
Nje kidogo ya Mji wa Songea, kipo kijiji kinachoitwa Mateka.
Bila shaka jina la kijiji hicho lina historia yake, lakini kubwa ni
kwamba ndiko anakoishi rubani wa ndege aliyeonja kifo kwa ajali ya ndege
na kifungo cha maisha.
Rubani huyu ni Kapteni Mstaafu Rodrick Robert (69)
mrefu, mweupe ambaye si mnene na wala si mwembamba akiwa na nywele
laini zinazoashiria wazi kwamba mmoja wa wazazi wake alikuwa mtu wa nje
ya Bara la Afrika.
Ni mara ya kwanza kumwona alipokuwa akifungua
mlango, lakini anatoka na tabasamu baada ya kuona wageni nje wakiwa na
mkewe aitwaye May Daud Robert aliyeniongoza kufika hapo mara ya pili
baada ya kumwomba aachie kidogo kazi yake mjini Songea na kunipeleka
nyumbani kwake nikaonane na mumewe.
Kwa kweli ilikuwa mara ya pili kwangu kufika pale
saa 11.00 jioni baada ya mara ya kwanza ya saa 4.00 asubuhi ya siku hiyo
kuwakosa nilipopelekwa na msamaria kwa pikipiki mbili.
Robert anatukaribisha ndani huku akisema alipata
taarifa za kuwapo kwa wageni wanaomtafuta tangu asubuhi. Tunaingia ndani
na kufika kwenye sebule ikiwa na makochi ya kawaida na hatimaye Robert,
mkewe na mimi tunaketi.
Akiwa anamwangalia mkewe aliyeketi upande wa kushoto kwake, Rubani Robert ananikaribisha.
Anasimulia kidogo historia yake.
Rubani: Nilizaliwa Mtaa wa Mtini mjini Songea
mwaka 1944 na baba yangu alikuwa mhandisi wa kujenga barabara na nyumba
za Serikali na alishiriki kujenga Uwanja wa Ndege za Jeshi Dar es
Salaam.
Nilisoma chekechea mjini Songea, Shule ya Msingi
Songea na Peramiho baadaye Sekondari ya Wavulana Songea kabla ya
kujiunga St Michael ya Iringa ambayo baadaye ikawa Mkwawa Sekondari na
sasa ni chuo.
Baada ya kumaliza Mkwawa nilingia Chuo Kikuu cha Dar e Salaam kuchukua Sayansi ya Jamii, lakini nilisoma mwaka mmoja nikaacha.
Mwandishi:Ni sababu zipi zilikuachisha chuo?
Rubani: Sikumbuki.
Post a Comment