Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahaman
Kinana
--
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahaman
Kinana amesikitishwa na taarifa ya kifo Cha Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko
ya Katiba Dr Sengondo Mvungi kilichotokea Jana katika Hospitali ya Millpark
nchini Afrika ya Kusini.
Kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi,
Katibu Mkuu anawapa pole wanafamilia, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko
ya Katiba, Jaji Warioba na Uongozi wa Chama Cha NCCR-Mageuzi. Hakika
Taifa limepoteza Mtaalamu wa Sheria, Kiongozi Mzalendo na hodari katika kipindi
ambacho mawazo yake yanahitajika kwa kiasi kikubwa kuliendeleza Taifa
hili.
Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi.
Imetolewa na:
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
ITIKADI NA UENEZI
13/11/2013
Post a Comment