John Mrema-Mkurugenzi wa Bunge na Halimashauri
CHADEMA .
--
·
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro aache kuvuruga Jumuiya
ya Afrika Mashariki
·
Watanzania wawezeshwe kushiriki fursa za soko la
pamoja la EAC na sio kuwazuia
·
Kampuni ya “Kilimanjaro Uchumi Company” isiwe na
hodhi ya kuuza mahindi Kenya.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Jana tarehe
12.11.2013 ziliandikwa taarifa za “Madereva wa Malori kugoma na shehena za
nafaka kukwama” katika mpaka wa
Tanzania na Kenya eneo la Holili kutokana na mpango wa Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro wa kuzuia wafanyabiashara kutoka Tanzania kwenda kuuza mahindi
Kenya na badala yake kuwataka waishie kwenye soko la Himo , huku akiruhusu
Kampuni moja ya ‘Kilimanjaro Uchumi Company’ kuwa na hodhi ya kusafirisha
mahindi hayo kutoka Himo kwenda Kenya .
Agizo hili la Mkuu wa mkoa kama alivyonukuliwa na
vyombo vya habari alisema kuwa “sisi tumesema wale wote wenye vibali vya
kuleta mahindi na mazao mengine wayauze soko la Himo halafu wafanyabiashara wa
Kenya ndiyo wayanunue hapo na kupeleka kwao Kenya”.
Agizo hili la mkuu wa Mkoa linaenda kinyume na
agizo la Rais Kikwete alilolitoa wakati akiwa kwenye ziara ya Kiserikali katika
mkoa wa Njombe kuwa ni ruksa wafanyabiashara wa Tanzania kusafirisha nafaka nje
ya nchi .
Aidha, katika wakati huu ambao tuko kwenye
kutafuta mtangamano mzuri baina ya nchi yetu na nchi wanachama wa EAC na wakati
ambao tunaelekea kuwa na itifaki ya soko la pamoja , sio busara hata kidogo
kuwanyima fursa watanzania kuweza kunufaika na masoko yaliyopo kwenye nchi za
Jumuiya ya EAC kwani hali hiyo itaendeleza utamaduni wa kuwafanya watanzania
kuwa nyuma ukilinganisha na wafanyabiashara wa nchi nyingine
Hivyo basi, tunaitaka serikali kuchukua hatua
zifuatazo ;
i.
Kuondoa mara moja zuio la Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro la kuwazuia wafanyabiashara wazawa kusafirisha mahindi yao mpaka
kwenye soko la Kenya
ii.
Serikali imchukulie hatua stahiki mkuu wa Mkoa kwa
kwenda kinyume na agizo la Rais ,na hasa kwa wakati huu ambao taifa lipo kwenye
mkakati wa kuondoa mapungufu yaliyojitokeza katika kutekeleza maazimio mbalimbali
vya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
iii.
Kuondoa hodhi kwa kampuni ya ‘Kilimanjaro Uchumi Company ltd’
ya kusafirisha mahindi kutoka Soko la Himo hadi Kenya na badala yake uchunguzi
ufanywe dhidi ya baadhi ya wamiliki wa kampuni hii kama wameshalipa deni la Halimashauri
ya Wilaya ya Moshi kiasi cha shilingi milioni 106 walilokuwa wanadaiwa kupitia
kampuni ya “Mafubilo Trading Company”
iv.
Pawepo na jitihada za makusudi za kuwawezesha
wafanyabiashara wa kitanzania kupata mitaji na mikopo nafuu ili waweze
kushindana na wale wa nchi jirani ili kuwawezesha kujiandaa kikamilifu kuingia
kwenye itifaki ya soko la pamoja la EAC.
Limetolewa na ;
…………………
John Mrema
Mkurugenzi wa Bunge na Halimashauri
CHADEMA .
Post a Comment