WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu
na Mbunge wa Monduli, mkoani Arusha, Bw. Edward Lowassa, ameisifu
Serikali ya Awamu ya Nne na kudai ndiyo iliyotekeleza Ilani ya Uchaguzi
ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kiwango kikubwa sana kuliko awamu
nyingine zilizopita.
Lowassa aliyasema hayo jana wakati
akihutubia mkutano wa hadhara baada ya kuweka jike la msingi la ujenzi
wa hospitali ya kisasa wilayani humo na kusisitiza kuwa, ujenzi huo ni
matokeo ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi. RAIS KIKWETE NA EDWARD LOWASSA KUSHOTO.
"Ndugu zangu wana
Monduli, huu ni uthibitisho wa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama
chenu, lazima niseme wazi kuwa, hakuna kipindi ambacho ilani hii
imetekelezwa kwa kiwango kikubwa kama awamu hii chini ya Rais Jakaya
Kikwete," alisema.
Hospitali hiyo ambayo majengo yake yatakamilika
Februari 2014, ujenzi wake utagharimu zaidi ya sh. bilioni mbili ikiwa
na uwezo wa kulazwa wagonjwa 72 katika wodi nne.
"Nilipotoa ahadi ya
kujenga hospitali hii, nilizingatia ilani ya CCM hivyo chama chetu
kinastahili pongezi na Rais Kikwete kwa kusimamia kidete ilani yetu ya
uchaguzi," alisema.
Lowassa aliongeza kuwa, hospitali hiyo ikikamilika itakuwa na vifaa vya kisasa na kuifanya moja ya hospitali bora nchini.
Alisema
alimfuata Rais Kikwete na kumuomba fedha kwa ajili ya mradi wa maji na
kupewa sh. bilioni tatu ambazo ziko benki ambapo msaada huo umelenga
kutimiza ilani ya CCM.
"Ndiyo maana nasema hakuna wamu ambayo
imetekeleza ilani ya uchaguzi kwa asilimia kubwa kama awamu hii ya Rais
Kikwete, pia Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), limeingia mkataba na
Halmashauri ya Wilaya ya Monduli.
"Mkataba huu ni wa ujenzi wa nyumba 100 na kati ya hizo, 50 zitapangishwa na nyingine za kuuza," alisema
on Friday, November 15, 2013
Post a Comment