mchango wao katika kuboresha afya ya mama na mtoto.
Tuzo
hizo zimeandaliwa na Taasisi ya Madaktari Waliosoma Vyuo Vikuu nchini
(THPI), na miongoni watakaopewa tuzo ni Rais Jakaya Kikwete, Rais
Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu
ya tatu, Benjamin Mkapa, mke wa Rais, Salma Kikwete na Mwenyekiti wa
makampuni ya IPP, Reginald Mengi
Kuhusu
THPI, ilianzishwa mwezi Machi, 2009 na madaktari 12, na Mkurugenzi wa
taasisi hiyo, Dk. Telesphory Kyaruzi, anasema wanaamini wakiwa wengi,
watahudumia watu wengi na jamii kubwa zaidi. Anasema, hadi sasa taasisi
ina madaktari wanachama zaidi ya 120 ambao wamesambaa nchi nzima.
"Lengo kuu la taasisi yetu ni kushiriki katika kuhamasisha uboreshaji
huduma za afya nchini na kushiriki kikamilifu katika kutoa huduma bora
za afya kwa watanzania,"anaongeza. Madaktari hao ni wale walioamua
kubaki nchini badalayakukimbilia nje
ya nchi kufanya kazi...kwa kifupi ni madaktari wazalendo.
"Tuliamua
kubaki nchini badala ya kwenda nchi za nje kutafuta maslahi mazuri
zaidi kwa sababu ya uzalendo juu ya nchi yetu. "Dira ya taasisi yetu,
tunaona watanzania wenye afya bora, huduma bora , na miundombinu bora
katika kutoa huduma za afya nchini . Katika taasis yetu nguvu yetu ni
umoja; wote ni sawa, kila mtu ni muhimu na kila mtu ni kiongozi. Nguvu
yetu ni matumaini,"anaongeza.
Dk.
Kyaruzi anasema ili kuwa na madaktari wengi sehemu mbalimbali nchini
wanaotoa huduma za afya, taasisi imeanzisha Idara ya Uendelezaji
Madaktari Vijana inayoratibu Mtandao wa Madaktari Vijana Nchini, ambao
ni Madaktari Wanafunzi( Medical Students), Intern Doctors, na Madaktari
wanaoanza kazi ili kuwajengea uwezo kitaaluma. Aidha, katika kutatua
matatizo ya afya nchini, anabainisha kuwa wanaongozwa na mpango
mkakati.
Katika
mpango wa mwaka 2011/2014, taasisi imejielekeza katika kutekeleza
malengo ya Milenia, lengo la nne na tano, afya ya mama na mototo. Na
kufikia lengo la kupunguza vifo vya akina mama kwa 75% ifikapo mwaka
2015. Katika kutekeleza jukumu hili muhimu, taasisi imeanzisha kampeni
ya kitaifa ya Saidia Mama Mjamzito Ajifungue salama, ili kupunguza vifo
vya mama na mtoto.
Kutokana
na taarifa za jarida la umoja wa mataifa , Global Health and Deplomacy,
duniani kina mama wajawazito 368,000 wanafariki kila mwaka, nafasi ya
mama mjamzito kufa ni mara 100 zaidi katika nchi zenye
idadi
kubwa ya vifo vya akina mama vinavyotokana na ujauzito. Akifafanua
hilo, Dk. Kyaruzi anasema kuwa ni nchi 21 tu duniani ziko kwenye hatua
sahihi katika kufikia malengo ya millennia ifikapo mwaka
2015.
"Vifo vya mama wajawazito nchini kwa mwaka 2005 vilikuwa ni 578, kwa
vizazi hai 100,000, na kufikia 454 kwa vizazi hai 100,000 kwa
mwaka 2012.
"Pia
vifo vya watoto chini ya miaka mitano vilikuwa 122 kwa watoto hai 1,000
mwaka 2004 mpaka 81 kwa watoto hai 1,000 mwaka 2012. Na vifo vya watoto
chini ya mwaka mmoja ilikuwa 68 kwa watoto hai 1,000 kwa
mwaka
2004 mpaka 51 kwa watoto hai 1,000 kwa mwaka 2012,"anasema. Kutokana na
juhudi kubwa za wadau, anasema wamefanikiwa kumepunguza idadi ya vifo
vitokanvyo na ujauzito na vifo vya watoto wachanga, lakini lazima
jitihada za kupunguza vifo vya mama na watoto ziedelee kwa nguvu kubwa
zaidi.
Ili
kutekeleza kampeni ya Saidia Mama Mjamzito ajifungue Salama, anasema
taasisi ilifanya utafiti wa awali, na kubaini upungufu wa damu ni namba
moja, ikifuatiwa na kifafa cha mimba, Aidha ni asilimia 50 tu ya
wajawazito wanaorudi kujifungua katika vituo vya afya, upungufu wa
mindombinu na maambukizi ya Kutoka kwa
mama
kwenda kwa mtoto ni changamoto kwa uzazi salama. "Kupitia kampeni
tunahamasisha wananchi kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wajawazito
wanaohitaji kwa dharura na kuhamasisha kina baba
kushiriki
katika afya ya uzazi ikiwa ni pamoja na kuwasindikiza kliniki ili
kujua dalili za hatari wakati wa ujauzito na kujiandaa kujifungua.
"Kuongeza
uwezo wa miundombinu katika utoaji huduma kwa mama wajawazito ambayo ni
matumizi ya simu kufuatilia mama mwenye dalili za hatari kupitia rafiki
kliniki mpaka anajifungua salama, kujenga wodi na vyumba vya dharura
(ICU) na Upasuaji (Theatres) pamoja na kuzuia maambukizi ya Virusi vya
UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto,"anaongeza. Akielezea kuhusu
tuzo, Dk. Kyaruzi anasema ya Rais Kikwete inatokana na jitihada
mbalimbali, na wanatambua kwa kuipa kipaumbele sekta ya afya.
Alipoingia
madarakani mwaka 2005, bajeti ya sekta ya afya ilikuwa ya sita, hivi
sasa ni ya tatu ikifuatiwa na miundombinu na elimu ambapo sekta hizi
zote zinategemeana huku afya ya mama na mtoto ni ya kwanza katika
vipaumbele vya Wizara ya Afya. "Rais ameunga mkono kampeni ya malaria
haikubaliki ili kulinda afya ya mama wajawazito na watoto wachanga,
katika kufanikisha malengo ya kupunguza vifo vya mama na mtoto duniani,
Umoja wa mataifa uliunda tume ya kuratibu taarifa na uwajibikaji juu ya
afya ya mama na mtoto na kumteua Rais Kikwete kuwa mwenyekiti mwenza
wa tume hii pamoja na Waziri Mkuu wa Canada .
"Hii
ni heshima kubwa kwa nchi yetu, ni imani kubwa dunia iliyonayo juu
yetu watanzania. Tuzo hii kwake ni ujumbe kwa jumuia ya kimataifa kwamba
na sisi watanzania tunamwamini Rais Wetu, tunamuunga mkono,"anaongeza.
Anaitaja tuzo ya Rais Mstaafu Mwinyi, kwamba imetokana na kazi nzuri
hasa kupinga maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na jitihada zake za mara kwa mara kuunga
mkono
matembezi ya hisani, kuwezesha upatikanaji wa fedha kusaidia watoto
wenye matatizo ya moyo na saratani ili wapate matibabu ndani na nje ya
nchi.
Mkapa
naye anapewa tuzo kwa kazi nzuri anayoifanya kupitia taasisi yake
ambapo Dk. Kyaruzi anasema, anafana kazi kubwa kujali afya ya mama na
mtoto. Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), nayo ni chanzo kikuu
kilichosababisha Mama Salma kupata tuzo kutoka madaktari hao.
Kwa mujibu wadk. Kyaruzi, Mengi anapata tuzo kutokana na utayari wake
kuisaidia jamii, kupitia vyombo vyake, Taasisi ya Madaktari Wanawake (MEWATA) wamefanya
kazi kubwa ya kuokoa maisha ya wakina mama kutokana na Saratani ya Matiti na Shingo ya
Kizazi.
Tuzo za kitaaluma zinaenda kwa Dk. Faraja Nipwapwacha, Daktari
Msaidizi , wa Kituo cha afya Kilimarondo mkoani Lindi , wilaya ya
Nachingwea, ambaye kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita hajapata
vifo vinavyotokana na uzazi.
"Uwezo
wake wa kujituma na tabia yake ya kufanya maamuzi sahihi kwa wakati na
haraka katika kuokoa maisha ya mama na mtoto, ametoa hamasa kubwa
kwamba tunaweza kuzuia vifo vinavyotokana na ujauzito ata sehemu
nyingine nchini,"anasema Dk. Kyaruzi. Anasema THPI inatambua kazi kubwa
inayofanywa na wauguzi nchini katika jitihada za kuboresha afya ya mama
na mtoto kupitia.
Muuguzi
ambaye amependekezwa na wauguzi wenzake kupitia chama chao kitaifa
cha TANNA ni Elia Mwumbui kutoka kijiji cha Matongo, kitongoji cha
Kimbiji, wilaya ya Ikungi, tarafa ya Ikungi Singida
vijijini kwa kuwa mfano wa wakina baba wanaoshiriki kusindikiza kliniki wake zao wajawazito.
Anasema
lengo ni kuhamasisha kuhusu afyaya mama na mtoto, kwani wanaamini
wajawazito na watoto wao wakiwa salama, taifa litakuwa salama na
tutajihakikishia ustawi kama Taifa. "Namshukuru Dk. Mary Nagu, Waziri
wa Uwezeshaji na Uwekezaji kwa kutuunga mkono, Dk. Asha Rose Migiro
kwa kuwa mlezi wa vijana wa THPI, taasisi na watu binafsi walioonyesha
nia ya kusaidia sehemu ya kampeni hii ya Saidia Mama Mjamzito ajifungue
salama inayoendeshwa na taasisi yetu ya THPI,"anaongeza.
Dk.
Kyaruzi anasema wana mradi wa kujenga uwezo kwa vituo vya afya katika
kuzuia maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa
mtoto katika Wilaya za Iringa Vijijini , Wangig'ombe na Mpanda na
umeandaliwa
kwa weledi wa hali ya juu na mshauri mkuu akiwa Dk. David Urassa,
unasubiri uwezeshaji wa fedha ili utekelezaji uanze.
"Pia
mradi wa ujenzi jengo la akina mama wajawazito kata ya Ikindilo, kituo
cha afya Ikindilo wilaya ya Itilima mkoa mpya wa Simiyu nao unasubiri
uwezeshaji wa fedha kuutekeleza,"anamaliza.
on Friday, November 22, 2013
Post a Comment