Balozi Hamisi Msumi
******
Viongozi hao tisa pasipo kutajwa majina yao na sehemu wanazoongoza ni pamoja na wabunge watatu, Mkurugenzi wa Jiji, Diwani, Mstahiki meya, Hakimu Mkazi mfawidhi, Mkurugenzi msaidizi, pamoja na Mkuu wa vitengo.
Miongoni mwa makosa wanayotumiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka, kushindwa kutoa tamko la Rasilimali na Madeni na kutoa tamko la uongo ikiwa ni kwa mujibu wa kifungu cha 6 na 15 vya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Namba 13 ya Mwaka 1995 kifungu 15 (a).
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Ofisa habari wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, kanda ya Tabora, Kajiru Shaban, ilieleza kuwa viongozi hao wanatarajiwa kuanza kuhojiwa na baraza hilo kuanzia leo hadi 22, mwaka huu mkoani Tabora.
Shabani alieleza kuwa baraza hilo liko chini ya Mwenyekiti wake, Balozi Hamisi Msumi na wajumbe wawili Celina Wambura na Hilda Gongwe.
Alisema baraza hilo linaketi kwa awamu ya tatu tangu kuanzishwa kwake na lina majukumu ya kupokea malalamiko kutoka kwa kamishna wa maadili ili kufanya uchunguzi wa kina pamoja na kumshauri Rais hatua za kinidhamu zinazopaswa kuchukuliwa dhidi ya viongozi wa umma wanaobainika kukiuka misingi ya maadili kwa mujibu wa sheria ya maadili.
Alieleza kuwa hatua hizo za kinidhamu zinaainishwa ba kifungu cha 8 cha sheria ya maadili kuwa ni pamoja na kuonywa na kupewa tahadhari, kushushwa cheo, kusimamishwa kazi na kufukuzwa kazi.
Nyingine ni kushauriwa kujiuzulu wadhifa unaohusu ukiukwaji huo, kupewa adhabu nyingine zinazoruhusiwa kwa mujibu wa sheria za nidhanmu kuhusu wadhifa wa kiongozi kwa mujibu wa kifungu cha 26(5) cha sheria ya maadili.
Alifafanua kuwa baraza litaendesha mashauri hayo hadharani hivyo kutoa fursa kwa wananchi kuweza kuhudhuria na kufuatilia.
CHANZO:
NIPASHE
Post a Comment