Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Wafanyakazi Strabag wagoma tena

 

Vibarua wa kampuni ya Strabag inayojenga barabara katika mradi wa magari yaendayo kwa kasi jijini Dar es Salaam (Darts), wamegoma kufanya kazi wakishinikiza kubadilishiwa bosi.
********
Vibarua wa kampuni ya Strabag inayojenga barabara katika mradi wa magari yaendayo kwa kasi jijini Dar es Salaam (Darts), wamegoma kufanya kazi wakishinikiza kubadilishiwa bosi.

Mgomo huo ambao ulianza jana saa 11:00 alfajiri, pia ulihusisha wafanyakazi wote walioajiriwa ambao wameungana na vibarua zaidi ya 100 kufunga mlango mkuu wa kuingilia katika ofisi za kampuni hiyo na hivyo kusababisha kazi zote kusimama.



Wafanyakazi wa kampuni hiyo waliwaambia waandishi wa habari kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya bosi wao (Strabag) kuingia mkataba na kampuni la Laba kukodi vibarua na kampuni hiyo ambayo pia inajihusisha na ujenzi wa barabara bila kupewa taarifa kamili.

“Tumeamua kugoma kutokana na unyanyasaji tunaopata kutoka kwa hawa wazungu, wameingia mkataba na watu wengine sisi hatujashirikishwa tunashangaa Jumamosi baada ya kupewa malipo yetu tunaambiwa tuongee na hao Laba ndiyo watakuwa wanatulipa sisi,” alisema Frank Michael, mmoja wa wafanyakazi.

Alisema kabla ya kuhamishiwa kwa Laba, walikuwa wakilipwa Sh. 17,500  kwa siku ambayo ilikuwa haiwatoshelezi kutokana na ugumu wa kazi wanazofanya na kupanda kwa gharama za maisha.

“Cha kushangaza Laba wao wamesema watatulipa Sh. 10,000 kwa siku na watalipa kwa njia ya Airtel Money, na jana (juzi), ndiyo walianza kufanya kazi rasmi na kuna baadhi ya vibarua ambao walifanya kazi chini yao wakalipwa Sh. 5,000 ya nusu siku,” alisema Michael.

Alisema baada ya juzi kuanza kufanya kazi chini ya kampuni ya Laba, waliamua kuomba kupewa maelekezo ya kutosha ili kufahamu mustakabali wao kutokana na baadhi yao wamefanya kazi za vibarua kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi kwenye kampuni hiyo, Abdullah Mahamood, alisema chanzo cha migogoro inayotokea mara kwa mara ni uongozi ambao umekuwa hauzingatii sheria na haki za wafanyakazi.

“Hii ni mara ya pili tangu kutokea kwa mgogoro hapa na chanzo ni huu uongozi ambao umekuwa haufuati sheria na kutumia mabavu kwenye haki kana kwamba kuna viongozi wa serikali ambao wako nyuma yao wanawalinda,” alidai Mahamood.

Alisema kampuni hiyo ilitakiwa kuwalipa madai yao ya nyuma kabla ya kuingia mkataba na kampuni nyingine ili kuondoa mgogoro ambao umesababisha kazi zote kusimama.

Naye Meneja Mkuu wa kampuni ya Laba, Emmanuel Mshana, alipoulizwa juu ya mkataba walioingia na Strabag, alisema wamekubaliana kupeleka vibarua kufanya kazi pamoja na kuwalipa.

“Kampuni hii imesajiliwa mwaka huu na Bodi ya Usajili ya Wakandarasi (CRB) kufanya kazi na kampuni za ujenzi wa barabara, kwa hiyo sisi tumeingia mkataba na Strabag kuwapelekea vibarua na kuwalipa na si vinginevyo,” alisema Mshana.

Uongozi wa Strabag ulipotafutwa kuzungumzia mgogoro huo, walinzi wa geti hilo waliwazuia  waandishi wa habari kuingia ndani kwa madai kuwa viongozi hawapo ofisini.
 

CHANZO: NIPASHE
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top