Baadhi ya wafanyabiashara walio katika maeneo
ya Kariakoo wamegoma kushiriki semina ya uelimishaji iliyokuwa itolewe
na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) katika kile walichokiita kupuuza
madai yao na kutaka kufanya vile wanavyotaka wao kuhusiana na sakata la
mashine za kielektroniki za kukusanyia mapato.
Mamlaka hiyo iliitisha mkutano katika Hoteli ya
Starlight ikilenga kuwaelimisha wafanyabiashara hao juu ya matumizi ya
mashine za kielektroniki, jambo ambalo lilizua zogo miongoni mwa
wafanyabiashara waliokuwepo katika eneo hilo.
Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa
wafanyabiashara wa nguo eneo la Kariakoo aliyekuwepo hotelini hapo,
akijitambulisha kwa jina moja tu la Mwanahamisi alisema siku ya Jumatano
gari la matangazo lilipita baadhi ya mitaa ya Kariakoo likiwataka
wafanyabiashara hao wafike kwenye mkutano uliopangwa kufanyika.
“Kutokana na taarifa hiyo kuletwa kienyeji, baadhi
ya wafanyabiashara wachache tumefika tukijua tutapata ufumbuzi juu ya
kilio cha muda mrefu kuhusiana na malalamiko waliyopeleka kwenye
mamlaka hiyo, a alisema.
Matokeo yake watu kutoka mamlaka hiyo waliofika
kwenye mkutano, walianza kutoa utambulisho juu ya kile walichotarajia
kukifanya ikiwa ni kutoa elimu juu ya matumizi ya mashine hizo.
MWANANCHI
MWANANCHI
Post a Comment