Watoto
wenye mahitaji maalum wanahitaji kupata ulinzi na mapenzi ya mara kwa
mara kutoka kwa walezi na jamii inayowazunguka ikiwa ni pamoja na kupata
nafasi ya kwenda shule kwani wengi wao wananyimwa fursa hiyo
ukilinganisha na watoto wengine.
Aidha mtoto akipata elimu ni
moja ya hatua ya mwanzo katika maendeleo ya taifa kwani baada ya
kuelimika atakuwa na ujuzi wa kitaaluma, kiteknolojia na raia mwenye
kufuata maadili ya nchi yake.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shule ya awali ya Carlton inayoongozwa na Mke wa Rais wa
Sri Lanka Mama Shiranthi Wickremasinghe Rajapaksa wakati wake wa
Marais na wakuu wa nchi na Serikali walipotembelea shule hiyo iliyopo
mjini Colombo jana ilionyesha kuwa shule hiyo inamtazamo wa kutoa elimu
kwa mtoto.
Elimu
ya shule hiyo ambayo hutolewa bure kwa watoto wenye mahitaji maalum na
wasio na mahitaji maalum imebuniwa kwa nia ya pekee ya kutoa elimu
sambamba na viwango vya kimataifa kwa watoto wan chi hiyo ambao
wanafundishwa kupitia njia rahisi ya nadharia na vitendo ambavyo
vinamfanya mtoto aweze kuelewa zaidi.
Shule
hiyo ilianza mwaka 1982 ikiwa na wanafunzi nane ambapo Mama Rajapaksa
alikuwa ni mmoja wa walimu wawili waliokuwepo ambao waliweza kutoa elimu
kwa watoto na kutokana na jitihada zake baadhi yao baada ya kumaliza
masomo wameweza kushika nyadhifa mbalimbali katika nchi hiyo ikiwa ni
pamoja na kuwakilisha Bunge la nchi.
Hasi sasa inamatawi nane yaliyopo katika mikoa mitatu ya nchi hiyo na
kuwa na zaidi ya watoto 2000 huku ikiwa na malengo ya kuendeleza utu
wa watoto, kutoa ujuzi wa uongozi, kuwawezesha watoto kuweza kujiamini
na kujithamini, kukuza stadi za watoto, kusimamia maadili na kurejesha
nidhamu kwa watoto.
Walimu
wa shule hiyo hufanya kazi ya kutambua vipaji vya watoto kwani huwapa
nafasi ya kuonyesha vipaji vyao katika matamasha ya mwisho wa mwaka na
hivyo kuweza kutimiza ndoto zao na kupatikana kwa viongozi wazuri katika
siku za usoni.
Wakiwa
shuleni hapo wake hao wa marais na wakuu wa Serikali walijionea michezo
mbalimbali iliyochezwa na watoto hao wenye umri wa chini ya miaka
mitano ikiwemo ngoma, kareti na kuogelea ambayo inawajenga kiakili na
kiafya na hivyo kuweza kufanya vizuri katika masomo yao.
Wake
hao wa Marais na wakuu wa serikali akiwemo Mke wa Rais Mama Salma
Kikwete walihudhuria mkutano wa 22 wa nchi wanachama wa Jumuiya ya
Madola (CHOGM) uliomalizika leo nchini humo.
Post a Comment